Sport
Dollar
40,2756
0.05 %Euro
46,8324
-0.27 %Gram Gold
4.321,0300
-0.26 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%AU imesema Rais Ndayishimiye ataongoza usaidizi mpya wa kidiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika na juhudi shirikishi zinazolenga kutatua changamoto za kiusalama na kibinadamu katika Sahel.
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, AU, ambaye pia ni rais wa Angola, João Lourenço, amemteua Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, kama Mjumbe wake Maalumu katika eneo la Sahel.
“Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika anamshukuru zaidi Rais wa Évariste Ndayishimiye kwa kukubali kazi hii ya kimkakati ya kisiasa kwa maslahi ya pamoja ya Muungano,” taarifa kutoka Umoja wa Afrika imesema.
AU imesema Rais Ndayishimiye ataongoza usaidizi mpya wa kidiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika na juhudi shirikishi zinazolenga kutatua changamoto za kiusalama na kibinadamu katika Sahel.
Hali tata ya usalama katika eneo la Sahel imechochewa na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utawala dhaifu, ulinzi duni mipakani, umaskini, na migogoro baina ya jumuiya. Makundi yenye itikadi kali hutumia udhaifu huu kuanzisha vituo, mashambulizi na kuajiri wafuasi katika eneo zima.
Michakato ya uongozi wa mpito inayoendelea katika eneo la Sahel, inayolenga kurejesha utulivu wa kikatiba kufuatia mapinduzi ya kijeshi huko Burkina Faso, Mali, na Guinea pia ni changamoto.
Rais wa Burundi ni Bingwa wa Umoja wa Afrika kwa Vijana, Amani na Usalama. AU huwapa majukumu marais tofauti kuendeleza sera zake ,na hapo kuwaita ”mabingwa” wa suala hilo.
Jukumu la Mjumbe Maalum linahusu kuimarisha mashirikiano na mamlaka za serikali, viongozi, watendaji na mashirika ya kikanda, mashirika ya kiraia na wadau wote husika ili kukuza mazungumzo, kujenga maafikiano, na kukuza mikakati ya kina kuelekea amani na utulivu wa kudumu ndani ya eneo la Sahel.
“Rais Ndayishimiye analeta pamoja naye tajiriba ya kisiasa, na sifa kamilifu za kujitolea kwa uthabiti kwa moyo wa Uafrika na ushirikiano wa kikanda . Uteuzi huo unaonyesha dhamira thabiti ya Umoja wa Afrika ya kusaidia ujenzi wa amani na ushirikiano wa kikanda katika mojawapo ya kanda muhimu zaidi barani Afrika,” Rais Lourenço wa Angola, Mwenyekiti wa AU amesema.
Comments
No comments Yet
Comment