Sport
Dollar
38,9164
0.11 %Euro
44,0481
-0.12 %Gram Gold
4.122,7300
-0.49 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Pesa hizi zilitolewa kupitia simu chini ya fungu maalumu la “Hustler Fund" mradi wa mikopo midogo midogo iliyoanzishwa na Rais William Ruto alipoingia madarakani 2022.
Serikali ya Kenya inapanga kufuta mikopo mibovu ya Ksh.6 bilioni iliyokopwa na Wakenya milioni 10 mwaka wa 2022.
Pesa hizi zilitolewa kupitia simu chini ya mfuko maalumu wa “Hustler Fund" mradi wa mikopo midogo midogo iliyoanzishwa na Rais William Ruto alipoingia madarakani 2022.
Taarifa ya serikali inasema kuwa watu waliokopa wameshindwa kulipa licha ya kukopa pesa hizo zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Biashara Ndogo Ndogo na za Kati nchini Kenya Susan Mag'eni alifika mbele ya Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Biashara, Viwanda na Ushirika, kuomba fedha zaidi.
"Hawajalipa kamwe, na hilo ndilo tutakalotaka kulifuta, kwa hivyo kwingineko ambako iko hatarini kabisa na ambayo haijalipwa ni takriban kati ya zaidi ya dola milioni 38 na dola milioni 46 (kati ya shilingi bilioni 5 na bilioni 6," Katibu huyo Mkuu aliwaambia wabunge.
Pia alitetea utendakazi wa hazina hiyo, ikionyesha kuwa wakopaji milioni 9 walikuwa wakikopa kikamilifu na kuwataka wabunge kuidhinisha ongezeko la dola milioni 38 (shilingi bilioni 5) katika hazina hiyo mwaka huu wa kifedha.
Mang'eni anasema kufikia sasa mikopo iliyotolewa kwa wananchi ni wametoa zaidi ya dola milioni 508 ( shilinmgi bilioni 65.7) huku wakopaji wakirejesha zaidi ya dola milioni 411 (Shilingi bilioni 53.2).
Licha ya deni hilo baya, alibainisha kuwa Wakenya milioni 9 wamelipa kikamilifu na kuongeza kikomo chao.
Ni kwa msingi huu ambapo Mang'eni aliwataka wabunge kuidhinisha nyongeza ya zaidi ya dola milioni 38 ( shilingi bilioni 5) kwa hazina hiyo katika mwaka ujao wa kifedha, wakati wanapofuatilia waliokiuka.
"Wale wanaofanya vyema zaidi - tunahitaji kuongeza kikomo chao. Na mara unapoongeza kikomo cha mtu kutoka dola nne hadi dollar 77 ( shilingi 500 hadi 10,000), tunapaswa kuwafadhili, na ndiyo maana tunaomba ufadhili wa ziada - kufadhili milioni 4.5 ambao watafuzu kwa daraja na wakati huo huo kutunza waombaji wapya ambao wanaingia kila siku katika Ufadhili," alisema.
Comments
No comments Yet
Comment