Sport
Dollar
38,8505
-0.06 %Euro
44,1336
0.1 %Gram Gold
4.157,9500
0.36 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Gladima anakuwa kiongozi wa tatu katika uongozi uliopita wa Macky Sall kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi.
Mahakama ya jijini Dakar imemtia hatiani waziri wa zamani wa madini wa Senegal, Aissatou Sophie Gladima kwa tuhuma za rushwa.
Kulingana na vyanzo vilivyokaribu na kesi hiyo, waziri huyo anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya Dola 330,000 kutoka kwa mfuko maalumu wa kuwahudumia wachimba madini walioathirika na maradhi ya Uviko-19.
Gladima anakuwa kiongozi wa tatu katika uongozi uliopita wa Macky Sall kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi.
Siku ya Jumanne, Mahakama ya Dakar ilimtia hatiani waziri wa zamani wa sheria wa Senegal Ismaila Madior Fall kwa tuhuma za kuomba rushwa.
Pia, ilimtia hatiani waziri wa zamani Salimata Diop kwa kuhusishwa na ufisadi.
Mawaziri wengine, Amadou Mansour Faye na Moustapha Diop, wanatarajiwa kupandishwa kizimbani katika siku zijazo.
Toka aingine madarakani mwaka jana, Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ameweka kipaumbele katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
Comments
No comments Yet
Comment