Dollar

38,8823

0 %

Euro

43,9831

0.06 %

Gram Gold

4.124,6600

0.38 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rigathi Gachagua anasema kuwa alipokea taarifa za kijasusi akidai kuwa rais wa nchi hiyo aligiza vyombo vya usalama kumuwekea sumu kupitia kemikali ambazo zitafanya ubongo wake kupooza katika muda wa miezi mitatu.

Kenya: Gachagua na siasa zake

Mamlaka za Kenya zimepuuzia madai ya aliyekuwa makamu wake wa rais, Rigathi Gachagua kwamba serikali ya Rais William Ruto inataka 'kummaliza.'

Gachagua anasema kuwa alipokea taarifa za kijasusi akidai kuwa rais wa nchi hiyo aligiza vyombo vya usalama kumuwekea sumu kupitia kemikali ambazo zitafanya ubongo wake kupooza katika muda wa miezi mitatu.

Oktoba 8, 2024, serikali ya William Ruto kupitia bunge la nchi hiyo, lilimng’oa madarakani Gachagua baada ya kutofautiana na bosi wake huyo, ambaye walishiriki pamoja katika kampeni ya mwaka 2022 na kutwaa uongozi.

Serikali ya Ruto imejibu vikali kauli za Gachagua, na kuziita za kikabila, pia kumtishia kumkamata.

Katibu wa Baraza la Mawaziri Kipchumba Murkomen na Naibu Rais Kithure Kindiki walimshutumu Gachagua kwa kuchochea mivutano ya kikabila na kutoa vitisho kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika kile walichokitaja kuwa ni jaribio la kuvuruga nchi ili kujinufaisha kisiasa.

"Hayuko juu ya sheria," Murkomen alisema wakati wa hafla ya umma huko Iten siku ya Jumamosi.

"Mwacheni mtu huyo aendelee kupiga kelele na kuwachochea Wakenya. Tutamkamata."

Haya yote yanazidisha joto la kisiasa nchini humo huku Gachagua akisisitiza kuwa atagombea Urais mwaka 2027.

Hivi karibuni, Gachagua alizindua chama chake kipya cha kisiasa, kiitwacho Democracy for the Citizens Party (DCP), alama yake ikiwa sikio na kauli mbiu ya: "Skiza Wakenya."

“Ifahamike kuwa chama chetu, DCP, kina uungwaji mkono halisi, na hatuwalipi wafuasi wetu kuhudhuria mikutano yetu jinsi serikali inavyowafanyia watu kuhudhuria mikutano yao,” alisema Gachagua katika mkutano wake na waandishi wa habari siku ya Jumatatu.

Kati ya sehemu ya viongozi wa chama cha DCP, ni pamoja na wale waliojikuta matatani na serikali ya William Ruto, akiwemo Waziri wa zamani wa Kilimo wa Kenya, Mithika Linturi ambaye alifutwa kazi mwaka 2022.

Wizara aliyoiongoza ilikumbwa na kashfa ya kuwauzia wakulima mbolea iliyochakachuliwa.

Kiongozi mwengine ndani ya DCP ni Cleophas Malala, ambaye, Agosti 2024 aliondolewa katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha UDA cha Rais William Ruto.

Gachagua anawaahidi Wakenya kile alichokiita "mtazamo mpya wa siasa za Kenya" zilizokita mizizi katika uwajibikaji kwa umma, kupambana na ufisadi, ushirikishwaji wa vijana na kutekeleza ahadi ambayo haijatekelezwa kikamilifu katika demokrasia halisi ya vyama vingi.

Tangu kuondolewa madarakani, Gachagua amekuwa akimkashifu bosi wake wa zamani kwa madai kuwa sio mkweli na kuwa na sera zisizofaa kwa maslahi ya Wakenya.

Hata hivyo, huku watu wengine wakiona chama kipya cha Gachagua kuwa pengine kinaweza kuleta ukombozi wa kisiasa, kuna wale ambao wamekuwa wakiwaza, je, uongozi wa Gachagua utakuwa na tofauti gani na ule wa Rais Ruto?

Na iwapo angekuwa bado yuko ndani ya serikali, angepata ujasiri wa kuikosoa?

Ikiwa imesalia miaka kadhaa kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2027, wengi wanasubiri kuona yatakayojiri baada ya kuundwa kwa chama hicho.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#