Dollar

38,8745

-0.01 %

Euro

43,9729

0.07 %

Gram Gold

4.111,8700

0.07 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rwanda imeandaa mkutano wa kujadili amani na usalama, wenye kuendesha mijadala ya kina juu ya changamoto za usalama za Afrika na kuhimiza suluhisho endelevu.

Kongamano la amani Rwanda lajadili mustakbali wa Afrika

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kuwa mustakabali wa Afrika, hasa masuala ya amani na usalama, hauwezi kutoka nje ya bara, akionyesha kwamba kwa muda mrefu sana, imekuwa ikichukuliwa kama mzigo wa kusimamiwa na wengine.

Kagame alikuwa akiongea katika Kongamano la Kimataifa la Usalama la Afrika (ISCA) mjini Kigali lililowaleta pamoja wajumbe kutoka nchi sabini, tarehe 19 na 20 Mei 2025.

Mkutano huo ni jukwaa la mijadala ya kina juu ya changamoto za usalama za Afrika na kuhimiza suluhisho endelevu.

Kati ya wanaohudhuria ni wataalamu wa masuala ya usalama na kijasusi, watunga sera, makampuni binafsi ya ulinzi na mashirika ya kiraia, miongoni mwa mengine.

“Usalama sio tu kukosekana kwa vitisho, kazi yetu kama viongozi ni kuunda mazingira ambayo watu wanaweza kuishi kwa heshima, kufurahia haki zao na kutazama siku zijazo kwa matumaini na ujasiri,” Rais Kagame aliuambia mkutano huo uliohudhuriwa na wataalamu wa masuala ya usalama na kijasusi, watunga sera, makampuni binafsi ya ulinzi na mashirika ya kiraia, miongoni mwa mengine.

Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na changamoto kubwa barani ya vita vinavyoendelea kama vile nchini Libya, Sudan Kusini, Sudan, na mizozo mipya inayosababisha kuongezeka kwa wimbi la uhamiaji na vifo.

“Hata kukiwa na mifumo bora ya ndani, hakuna nchi inayoweza kujilinda kwa kutengwa. Vitisho visivyo na mipaka kama vile magonjwa ya milipuko, ugaidi na uhalifu wa mtandaoni hubadilika haraka sana mara nyingi zaidi kuliko majibu ya kitaifa lakini ushirikiano lazima upite zaidi ya kupeana habari tu,” aliongezea.

Martin Kimani, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Afrika huko New York, Marekani aliangazia jukumu la Umoja wa Mataifa, UN, kwa kuzuia vita vikubwa kati ya mataifa makubwa.

Alibainisha kuwa UN imefanikiwa kwa njia za msingi zaidi za masharti yake, hata hivyo imeshindwa ahadi yake ya kusimamisha vita mahali pengine na imetumiwa kuwakinga washirika wa mataifa makubwa wakati wanafanya vitendo vya ukatili.

"Baraza la usalama limetumika kama jukwaa la kuanzisha mashambulizi dhidi ya maslahi ya Afrika. Kwa mfano mashambulizi ya Libya."

Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Umoja wa Afrika, ambae pia amehudhuria mkutano huo anasema kuwa miaka 14 baada ya Libya kuingiliwa, hakuna serikali.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#