Sport
Dollar
38,9222
0.13 %Euro
44,0561
-0.1 %Gram Gold
4.127,5700
-0.37 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Boniface Mwangi wa Kenya na mwanaharakati mwenzake wa Uganda Agather Atuhaire walikamatwa na mamlaka za Tanzania siku ya Jumatatu walipokwenda nchini humo wakitaka kuhudhuria kesi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu.
Wizara ya Mambo ya Nje nchini Kenya imeitaka serikali ya Tanzania kumuachilia mwanaharakati Boniface Mwangi au kutoa nafasi kwa yeye kupata msaada wa kisheria au kuonana na wawakilishi kutoka ubalozi wa nchi yake.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya inaelezea wasiwasi wake kufuatia kuendelea kuzuiliwa kwa raia wa Kenya, Boniface Mwangi na Serikali ya Tanzania,” imesema sehemu ya taarifa iliyotolewa Mei 21, na pia kuwekwa kwenye mtandao wa X wa Wizara hiyo.
Jaji Mkuu mstaafu wa Kenya David Maraga ameilaumu serikali ya Kenya kwa kushindwa kutoa msaada kuhakikisha kuwa mwanaharakati huyo ameachiliwa huru.
Maraga anasema kuendelea kuzuiliwa kwake nchini Tanzania ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.
‘’Nimesikitishwa kwa kuendelea kuzuiliwa kwa Boniface Mwangi na mamlaka za Tanzania bila ya kufikishwa mahakamani, kupata ushauri wa kisheria au kuonana na mwakilishi wa ubalozi, hii ikiwa ni ukiukwaji wa wazi wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu,’’ Maraga alisema.
‘’Nailaumu serikali ya Kenya kwa kushindwa kulipa umuhimu suala la kuhakikisha kuwa Boniface Mwangi ameachiliwa mara moja bila masharti yoyote,’ aliongeza Jaji Mkuu mstaafu Maraga.
Boniface Mwangi wa Kenya na mwanaharakati mwenzake wa Uganda Agather Atuhaire walikamatwa na mamlaka za Tanzania siku ya Jumatatu walipokwenda nchini humo wakitaka kuhudhuria kesi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu.
Licha ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kukemea vitendo vya wanaharakati kutoka nchi jirani kuingia katika taifa lake na kufanya shughuli za uanaharakati, serikali haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na kuzuiliwa kwa wanaharakati hao.
Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wanaharakati nchini Kenya, wanaotaka serikali ichukue hatua zaidi za kuhakikisha wenzao hao wawili wanaachiliwa mara moja, huku wengine wakiilaumu serikali ya Kenya kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti.
Comments
No comments Yet
Comment