Sport
Dollar
41,4534
0.14 %Euro
48,6966
-0.55 %Gram Gold
4.971,3000
-0.76 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Aliwania wadhifa wa juu nchini mwaka 2021 lakini akashindwa na Rais aliye madarakani Yoweri Museveni.
Dunia ilimfahamu kama Bobi Wine tangu miaka ya 2000 alipong’aa katika fani ya muziki.Robert Kyagulanyi mzaliwa wa 1982, ameteuliwa rasmi na tume ya Uchaguzi ya Uganda kugombea urais mwaka wa 2026 kupitia Chama cha National Unity Party (NUP).
Bobi Wine alijizoelea umaarufu kwa nyimbo zake zilizoangazia maswala ya kijamii na kutetea haki za wananchi wa chini alijipatia jina maarufu la “Ghetto president”.
Alilelewa katika makazi ya mabanda ya Kamokya jijini Kampala na hili lilichangia pakubwa kwa ujumbe ambao muziki wake ulitoa, ujumbe wa kuleta burudani na kuelimisha.

Bobi Wine aliingia katika siasa 2017 alipokuwa mgombea huru katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Kyadondo Mashariki na kushinda.
Mnamo Agosti 2018, Wine alikamatwa na kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi, ambapo alishtakiwa kwa kupatikana na bunduki kinyume cha sheria.
Akiwa kizuizini ililazimika apate huduma ya afya nchini na baadaye akapewa rufaa kwenda nje ya nchi, lakini akakamatwa tena aliporejea Uganda mwezi mmoja baadaye. Baada ya muda serikali ikamuachia.
Mnamo tarehe 24 Julai 2019, alitangaza rasmi azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2021 chini ya Chama cha Umoja wa Kitaifa.
Aliwania wadhifa wa juu nchini mwaka 2021 lakini akashindwa na Rais aliye madarakani Yoweri Museveni.
Bobi Wine sasa anajaribu kwa mara ya pili katika nafasi hiyo akionekana kama mpinzani mkuu wa Rais Museveni ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu 1986, akiwa tayari ametangaza nia ya kuwania tena urais kwa muhula wa saba.
Bobi Wine anaelezea msingi wake wa kutaka uongozi wa nchi 2026 kama muendelezo wa "dhamira yake ambayo haijakamilika".
Comments
No comments Yet
Comment