Dollar

41,4187

0.12 %

Euro

48,9536

0.16 %

Gram Gold

5.013,9700

0.61 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Wanyama hao walianguka kutoka kwenye mwamba hadi ndani ya mto na wengine wakakanyagana, kulingana na wizara ya utalii.

Karibu nyati 100 waliokuwa wanakimbia simba wafariki kutokana na mkanyagano

Nyati wasiopungua 90 walikanyagana hadi kufariki siku ya Jumanne wakati wakikimbia simba nchini Namibia, maafisa wa wanyamapori wamesema.

Mkanyagano huo ulitokea karibu saa kumi na moja asubuhi karibu na Mto Chobe, katika eneo la hifadhi la Zambezi.

Simba hao waliwafukuza nyati kutoka nchi jirani ya Botswana, msemaji wa wizara ya utalii Ndeshipanda Hamunyela aliliambia shirika la AFP.

‘‘Ni masikitiko makubwa kuhusu tukio hili. Wanyama walianguka kutoka kwenye mwamba mrefu hadi ndani ya mto na wengine wakakanyagana," alisema.

Video iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii na Shirika la Habari la Taifa la Namibia inaonesha wanaume kadhaa wakiwa na mashoka huku wakikata nyama kutoka kwa mizoga ya nyati.

Namibia, nchi ya Afrika ambayo ina sehemu kubwa ya jangwa, inaingiza asilimia saba ya mapato yake kutokana na utalii.

Mwaka 2018, nyati zaidi ya 400, ambao wanaaminika walifukuzwa na simba, walizama ndani ya mto kaskazini mwa Botswana.

Si kawaida kwa nyati kuzama ndani ya mto katika eneo hilo, lakini idadi yao huwa ni ndogo sana.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#