Dollar

41,3612

-0.04 %

Euro

48,8519

0.43 %

Gram Gold

4.980,8300

1.58 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mamlaka zinasema kuwa watu wasiojulikana na waliokuwa na silaha waliwalenga maafisa hao eneo la Agu la Jimbo la Benue; washukiwa 6 wamekamatwa

Polisi 3 wauawa, 7 watekwa nyara katika shambulio la silaha Nigeria

Maafisa watatu wa polisi wameuawa na wengine saba kutekwa nyara siku ya Jumapili katika shambulio la silaha Jimbo la Benue nchini Nigeria, maafisa wanasema.

Benjamin Hundeyin, afisa uhusiano mwema wa Polisi nchini Nigeria, alisema katika taarifa kuwa watu wasiojulikana na waliokuwa na silaha waliwalenga maafisa wa polisi katika eneo la Agu.

Hundeyin alithibitisha kuwa maafisa watatu walipoteza maisha wakati wa shambulizi hilo huku saba wakitekwa nyara. Aliongeza kuwa maafisa wa usalama wamepelekwa kwenye eneo hili na washukiwa saba tayari wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#