Dollar

41,3771

0 %

Euro

48,7445

0.21 %

Gram Gold

4.955,8100

1.07 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Serikali ya Kenya imetangaza rasmi mashirika ya Muslim Brotherhood na Hizb-ur-Tahrir kuwa mashirika ya kigaidi chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi (Kipengele cha 59B).

Kenya yaitangaza Muslim Brotherhood na Hizb-ur-Tahrir kuwa makundi ya kigaidi

Tangazo hilo limetolewa kupitia Notisi ya Kisheria No. 157 iliyochapishwa kwenye Kiambatisho cha Gazeti Rasmi la Serikali la Kenya tarehe 19 Septemba 2025, likitolewa na Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, chini ya Kifungu cha 3(3) cha sheria hiyo.

Agizo hilo, linalojulikana kama Agizo la Kuzuia Ugaidi, 2025, linaanza kutumika mara moja na litaendelea kuwa hivyo hadi pale litakapotenguliwa na Waziri au Mahakama.

Agizo hilo linafanya kuwa kosa la jinai kuwa mwanachama, kuunga mkono, kuchangisha fedha, au kueneza propaganda inayohusiana na mashirika hayo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#