Dollar

41,4087

0.1 %

Euro

48,9468

0.13 %

Gram Gold

5.021,1400

0.76 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Kenya William Ruto amesema kikosi ambacho kimekuwa kwenye majukumu hayo kwa miezi 15 - kinachojulikana kama ujumbe wa Multinational Security Support - kimekuwa kikifanya kazi kwa asilimia 40 pekee ya uwezo wa walinda usalama 2,500.

Kenya yaomba msaada zaidi kwa ujumbe wa amani Haiti

Marekani ilitaka kuungwa mkono katika Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu (Septemba 22) kwa ajili ya upanuzi wa kikosi cha kimataifa kukabiliana na magenge ya watu wenye silaha nchini Haiti, kwa kuzingatia ujumbe unaoongozwa na Kenya ambao Rais wa Kenya William Ruto alisema ulikuwa na uhaba wa maafisa na vitendea kazi.

Magenge yenye silaha yamechukuwa udhibiti wa karibu mji mkuu wote wa Haiti Port-au-Prince katika mzozo ambao umewalazimu takriban watu milioni 1.3 kuyahama makazi yao, kuua maelfu ya watu na kusababisha baa la njaa kwa kiwango kikubwa.

Katika hafla iliyoandaliwa na Marekani na Kenya pembeni mwa mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa wa viongozi wa dunia, Rais Ruto alisema kikosi hicho ambacho kimekuwa kwenye majukumu hayo kwa miezi 15 - kinachojulikana kama ujumbe wa Multinational Security Support - kimekuwa kikifanya kazi kwa asilimia 40 pekee ya uwezo wa walinda usalama 2,500.

Muda wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ujumbe wa MSS unakaribia kufikia mwisho tarehe 2 Oktoba.

Azimio la Baraza la Usalama linahitaji angalau kura tisa za ndio kati ya 15 na hakuna kura ya turufu ya Marekani, Uingereza, China, Ufaransa au Urusi.

"Lazima niipongeze Marekani. Waliwezesha kupatikana kwa vitendea kazi na magari. Lakini kwa bahati mbaya, magari mengi yalikuwa yametumika na kwa hivyo mara nyingi yalikuwa yanaharibika. Na kwa kweli, iliweka maafisa wetu katika hatari kubwa wakati yanaharibika katika maeneo hatari sana," Ruto alisema.

"Lakini angalau walipiga hatua," aliongeza.

"Hata hivyo hatukupata usaidizi wowote muhimu kutoka kwa sehemu nyingine yoyote." Marekani na Panama mwezi uliopita ziliwasilisha rasimu ya azimio la kubadilisha misheni iliyopo ya MSS ya miezi 15 kuwa Kikosi kipya cha Kukabiliana na Magenge kinachoungwa mkono na ofisi mpya ya Umoja wa Mataifa.

Kikosi kipya kilichopendekezwa bado kingetegemea michango ya hiari ya kimataifa ya wafanyakazi na ufadhili, lakini muundo wa uongozi ungekuwa tofauti.

Itaongozwa na kundi la wawakilishi kutoka nchi ambazo zimechangia maafisa, pamoja na Marekani na Kanada.

Pendekezo hilo linafuatia msukumo ulioongozwa na Marekani mwaka jana kubadilisha ujumbe unaoongozwa na Kenya kuwa kikosi rasmi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa ili kuimarisha rasilimali zake, jambo ambalo lilipingwa na Urusi na China.

"Haiti iko katika njiapanda. Port-au-Prince inakabiliwa na mzozo unaoongezeka wa usalama huku magenge yakifanyia jamii ugaidi, kunyang'anya familia na kuajiri watoto waliokata tamaa kufanya mambo ya kutisha kwa niaba ya viongozi wa magenge," alisema Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Christopher Landau, ambaye pia alitangaza kuwa Marekani ilikuwa ikiwawekea vikwazo maafisa wawili wa zamani wa Haiti.

Alisema MSS haina "mamlaka na rasilimali zinazohitajika kushughulikia ukubwa wa changamoto" nchini Haiti.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#