Sport
Dollar
41,4601
0.15 %Euro
48,7097
-0.52 %Gram Gold
4.993,3700
-0.32 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Akiwa amezaliwa Aprili 5, 1955, Rais Chakwera alitumia muda mrefu wa maisha yake kama mwanateolojia na kwa nyakati tofauti amehudumu kama ‘baba mchungaji’ kabla ya kuingia kwenye ulingo siasa za Malawi mwaka 2013.
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amekubali matokeo ya uchaguzi wa Urais ambayo yamempa ushindi kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Peter Mutharika.
Katika hutoba yake ya Septemba 24, 2025, Chakwera amesema amekubali matokeo na yuko tayari kwa makabidhiano ya madaraka, kufuatia uchaguzi wa Septemba 16.
"Ni vyema nikakubali kushindwa kulingana na matakwa ya raia wetu na kwa kuheshimu katiba yetu," alisema Rais Chakwera siku ya Jumatano.
Akiwa amezaliwa Aprili 5, 1955, Rais Chakwera alitumia muda mrefu wa maisha yake kama mwanateolojia na kwa nyakati tofauti amehudumu kama ‘baba mchungaji’ kabla ya kuingia kwenye ulingo siasa za Malawi mwaka 2013.
Alijipenyenza kwenye siasa akiwa kama kiongozi wa chama cha upinzani cha Malawi Congress Party (MCP), ambacho kilihusika na kuuangusha utawala wa Kiingereza mwanzoni mwa miaka ya 60.
Ikumbukwe kuwa, Baba Mchungaji Chakwera aliwania kiti cha urais mara mbili, mwaka 2014 na 2019, akishika nafasi ya pili kwa nyakati mbalimbali.
Akishirikiana na aliyekuwa mgombea mwenza wake Saulos Chilima, Baba Mchungaji Chakwera, aliongoza umoja wa Tonse, ambao uliundwa na vyama tisa vya upinzani, kuondoa madarakani utawala wa rais Mutharika.
Wakati akiwania nafasi ya urais, Chakwera alijinasibu kuwa yeye ni mtumishi wa watu, aliyeazimia kuunganisha Wamalawi wote, kukomesha ufisadi na kukuza uhuru wa mahakama na utawala wa sheria.
Comments
No comments Yet
Comment