Sport
Dollar
40,3906
-0.01 %Euro
47,3036
0.54 %Gram Gold
4.412,8500
1.43 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais William Ruto wa Kenya anasema kuwa anasingiziwa na kwamba, aliahidi tu kinachoweza kufanyika wala hazikuwa ahadi za kupitiliza bali ni kuinua matumaini ya Wakenya.
Rais wa Kenya William Ruto, anaonekana kuandamwa na jinamizi la ahadi hewa anazodaiwa kutoa wakati wa kampeni yake ya urais.
Miongoni mwa ahadi hizo, ilikua ni pamoja na kutengeza ajira zaidi ya milioni 4, pamoja na kuinua kipato na maisha ya walala hoi.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki Rais Ruto ameendelea kuitetea serikali yake huku akisema kuwa Wakenya wamekuwa wakimlaumu kwa kutoa ahadi nyingi anazoshindwa kutimiza.
Rais Ruto anasema kuwa anasingiziwa na kwamba, aliahidi tu kinachoweza kufanyika wala hazikuwa ahadi za kupitiliza bali ni kuinua matumaini ya Wakenya.
“Nitatimiza ahadi zote nilizozitoa katika muhula wangu huu,” alisema Rais Ruto mwishoni mwa juma, alipokuwa akiongea na waumini katika Kaunti ya Machakos.
Lakini Wakenya, hasa Gen Z wameendelea kushikia bango, na kuibua maswali mengi hasa katika maandamano ya hivi karibuni.
Kubwa ikiwa ni utendaji kazi wa serikali lakini zaidi ahadi zilizotolewa na uongozi wa serikali hiyo hasa wakati wa kampeni za uchaguzi 2022.
Rais Ruto anadai maandamano ambayo yamekuwepo hivi karibuni nchini Kenya yana malengo ya kisiasa yakitumia mtaji wa vijana ambao hawana ajira kufikia maslahi yao binafsi.
Katika tukio hilo hilo, Rais Ruto, aliwataka wazazi, kuwalea watoto wao vizuri huku akisema kuwa yeye anatenga muda wa kuongea na watoto wake.
“Polisi wamepewa mafunzo ya kukabiliana na wahalifu, hawajafunzwa kulea watoto. Sijui mnatarajia nini mnapowaachia watoto wenu polisi? Kila mzazi, mimi nikiwemo, nachukuwa muda wa kuwalea watoto wangu, na kwa hiyo ni jukumu la kila mtu,’’ William Ruto, Rais wa Kenya.
Sasa hivi Kenya inakadiriwa kuwa na ukosefu wa ajira wa asilimia 12.7.
Miongoni mwa vijana wa kati ya umri wa 15 na 34, ambao wanawakilisha asilimia 35 ya idadi ya raia wa Kenya, asilimia 67 kati yao hawana ajira.
Pamoja na kuwa anadai serikali yake imeweka mpango mkakati wa kupatikana kwa ajira, lakini vijana bado wanahisi hiyo pia inachangia katika ahadi hewa.
Kwa upande wake, aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Raila Odinga amependekeza suluhu ya kukutana na wawakilishi wa Gen Z na viongozi wengine kutoka kote nchini.
Raila anasema maandamano hayawezi kuwa tiba ya matatizo na kinachotakiwa kwa sasa ni majadiliano. Haifahamiki ni nani atakayewakilisha kundi hilo la Gen Z kwa sababu siku zote, limekuwa likiratibu maandamano yake kupitia mitandano ya kijamii bila kuwa na kiongozi rasmi.
Pengine hili litakuwa funzo kwa wanasiasa wengine, kwani Waswahili wanasema, bora kujikwaa kidole kuliko ulimi, lakini pia unaposema, basi usimalize maneno.
Comments
No comments Yet
Comment