Dollar

40,4366

0.06 %

Euro

47,6116

0.05 %

Gram Gold

4.414,8900

0.08 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Uturuki Erdogan asema "hatamuacha al Sharaa peke yake", akiongeza kuwa kujengeka upya kwa Syria kutanufaisha Uturuki.

Erdogan aapa kumuunga mkono al-Sharaa, anakataa kugawanywa kwa Syria

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitiza kumuunga mkono mwenzake wa Syria, na kuapa "kutomuacha al-Sharaa peke yake", amekataa mgawanyiko nchini Syria, na kusema kujengeke upya kwa nchi hiyo iliyokumbwa na vita ni manufaa kwa Uturuki.

"Wakati ambapo hata watendaji wasiotarajiwa wanakutana pamoja kuhusu Syria, ni muhimu kuueleza ulimwengu Israel inavuruga juhudi za kurejesha utulivu," Erdogan aliwaambia waandishi wa habari kwenye ndege yake ya kurejea kutoka Jamhuri ya Uturuki ya Kupro Kaskazini (TRNC) mwishoni mwa siku ya Jumapili.

Ankara imeunga mkono uanzishwaji wa serikali ya mpito nchini Syria unaoongozwa na Rais Ahmed al Sharaa, ambaye alichukua madaraka baada ya kuanguka kwa utawala wa Assad mnamo Desemba 2024.

Katika kusitishwa kwa mapigano huko Sweida nchini Syria, mji ambao hivi karibuni ulishuhudia mapigano kati ya makabila ya Bedouin na jamii ya wachache wa Druze na baadaye uingiliaji kati kwa Israeli, Erdogan alisema mwenzake wa Syria ameshikilia msimamo thabiti, bila kuonyesha nia yoyote ya kuyumba hadi sasa.

"Israel haitaki utulivu katika eneo hilo. Inaamini kuwa Syria iliyoungana sio kwa maslahi yake na kwa hivyo inaendeleza na vitendo vya uchokozi," aliongeza.

Kuhusu suala la Kupro, kiongozi wa Uturuki alisema hana mpango wa kutembelea Kupro Kusini, akisisitiza: "Kama vile hawatambui TRNC kama nchi, hatuitambui Kupro Kusini kama nchi."

Alikariri kwamba ufunguo wa kusuluhisha mzozo wa Kupro upo katika suluhisho la mataifa mawili, na kwamba hakuna nafasi ya kubadili msimamo huo kwa njia yoyote ile.

Kuhusu ununuzi wa ndege za Eurofighter kwa Uturuki, Erdogan alisema Uingereza na Ujerumani zimechukua msimamo "chanya".

Alisema Umoja wa Ulaya haupaswi kusubiri hata siku moja kufufua na kuendeleza mazungumzo ya kujiunga kwa Uturuki.

Kuhusu vita vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza, Erdogan alisema anaamini kuwa watu wa Gaza hawatasalimu amri, akisisitiza kwamba "Israel inafanya mashambulizi kama mnyama aliyechanganyikiwa, na itajiangamiza kwa ghadhabu hii".

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#