Dollar

40,4228

0.06 %

Euro

47,3391

-0.01 %

Gram Gold

4.405,4400

-0.14 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Ukraine Zelenskyy anasema mkutano unaofuata na Urusi unapaswa kuzingatia kurejea kwa POW, kurejeshwa kwa watoto waliotekwa nyara, na kuandaa mazingira ya mkutano wa viongozi.

Ukraine inapendekeza mazungumzo mapya ya amani na Urusi kufanyika Uturuki

Ukraine imependekeza kufanyika kwa duru inayofuata ya mazungumzo na Urusi nchini Uturuku, huku Rais Volodymyr Zelenskyy akisema mkutano huo unafaa kushughulikia kurudishwa kwa wafungwa wa vita, kurejeshwa kwa watoto wa Ukraine waliopelekwa Urusi, na kujengwa msingi wa mkutano wa kilele unaotarajiwa wa viongozi wa nchi hizo mbili.

Akizungumza na mabalozi wa Ukraine mjini Kiev siku ya Jumatatu, Zelenskyy alisema Rustem Umerov, mkuu wa Baraza la Usalama la Taifa la Ukraine, alitoa pendekezo hilo, akisisitiza kwamba "mazungumzo yenye ufanisi yanaweza tu kufanyika katika ngazi ya viongozi wa kitaifa."

Aliwataka wanadiplomasia kupata msaada wa kimataifa kwa muundo huo.

"Ajenda kutoka upande wetu iko wazi," Zelenskyy alisema kupitia mtandao wa X.

"Ninawasihi muzifahamishe nchi wenyeji juu ya umuhimu wa mfumo huu wa mazungumzo."

Je, vipaumbele muhimu vya Ukraine ni gani?

Wakati Ukraine inapojiandaa kwa duru ya tatu ya mazungumzo, Zelenskyy alielezea vipaumbele muhimu vya kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na kupanua vikwazo vya kimataifa dhidi ya Urusi, kupata mifumo zaidi ya ulinzi wa anga, na kuongeza usambazaji na ufadhili wa ndege zisizo na rubani.

Alisema kuwa Ukraine imepata ushirikiano wa kimataifa ambao haujawahi kushuhudiwa, hata hivyo miundo mipya inahitajika.

"Kuanzia mfano wa Denmark, hadi juhudi za Czech katika masuala ya mizinga, na ndege za kivita za Mirage kutoka Ufaransa zinazosaidia kuimarisha uwezo wetu wa anga... sasa kipaumbele ni matumizi ya ndege zisizo na rubani – za aina zote," alisema.

Akitaja mali za Urusi zilizogandishwa pamoja na ushindi wa Ukraine katika kesi za kimataifa, alisisitiza haja ya ubunifu katika kuzigeuza kuwa rasilimali za kuisaidia Ukraine katika ulinzi wake.

Pia alitaja uratibu unaoendelea na utawala wa Rais Donald Trump juu ya ulinzi wa anga na mipango ya pamoja ya ndege zisizo na rubani.

Zelenskyy alisisitiza zaidi ushirikiano wa Ukraine zaidi ya NATO na EU, akitaja miundo kama vile Ukraine-Ulaya ya Kaskazini, Ukraine-Ulaya ya Kusini-Mashariki, na Jukwaa la Crimea, pamoja na ushirikiano maalum na Uturuki.

Siku ya Jumamosi, rais wa Ukraine alisema Kiev ilipendekeza duru mpya ya mazungumzo ya amani na Urusi "wiki ijayo," akisisitiza umuhimu wa mkutano wa viongozi ili kuendeleza juhudi za amani, akisema Ukraine iko tayari.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#