Sport
Dollar
40,4319
0.06 %Euro
47,3816
0.09 %Gram Gold
4.417,2800
0.13 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Ankara inasema hatua ya Athens kutangaza iifadhi za baharini katika maji ya Aegean haina uzito wa kisheria, ikihimiza ushirikiano badala ya hatua za upande mmoja katika Bahari ya Aegean na Mediterania.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imeelezea msimamo wake kuhusu uamuzi wa Ugiriki kutangaza hifadhi mbili za baharini katika bahari za Aegean na Ionia, ikisisitiza kwamba “inapaswa kuepukwa kuchukua hatua za upande mmoja katika maeneo ya bahari yaliyofungwa au ya yaliyofungwa nusu kama vile bahari ya Aegean na Mediterania.”
Wizara ilibainisha kwamba hatua ya Ugiriki, iliyotangazwa mwaka jana, haitakuwa na madhara yoyote ya kisheria, hasa ikizingatiwa kwamba bado kuna masuala ya Bahari ya Aegean ambayo hayajatatuliwa kati ya nchi hizo mbili, yakiwemo maeneo ya kijiografia ambayo umiliki wake haujakabidhiwa kwa Ugiriki kupitia mikataba ya kimataifa.
Wizara hiyo ilirejelea taarifa yake ya tarehe 9 Aprili 2024 iliyosisitiza msimamo huo, na kueleza kuwa maoni yaliyotolewa wakati huo bado ni sahihi hadi leo.
"Sheria ya kimataifa ya bahari inahimiza ushirikiano, ikiwa ni pamoja na masuala ya mazingira, kati ya mataifa ya pwani katika bahari iliyofungwa au iliyofungwa nusu. Katika muktadha huu, tunasisitiza kwamba Uturuki inasalia kuwa tayari kushirikiana na Ugiriki, kama moja ya mataifa mawili ya pwani katika Bahari ya Aegean," taarifa hiyo ilisema Jumatatu.
Wizara ilisistiza kwamba jitihada za kutumia maadili ya kimataifa kama ulinzi wa mazingira katika muktadha wa masuala yanayohusiana na Bahari ya Aegean, pamoja na hadhi ya visiwa, visiwa vidogo na miamba ambayo umiliki wake haujakabidhiwa kwa Ugiriki kupitia mikataba ya kimataifa, hazitazaa matokeo yoyote ya kisheria, sawa na ilivyokuwa huko nyuma.
"Uturuki itatangaza miradi yake ya ulinzi wa mazingira katika maeneo yake ya baharini katika siku zijazo," iliongeza.
Taarifa hiyo pia ilisisitiza msimamo wa Uturuki kwamba mtazamo wa dhati na wa kina unapaswa kupitishwa ili kutatua masuala kwa kuzingatia sheria ya kimataifa, usawa, na ujirani mwema, chini ya Azimio la Athens la Desemba 7, 2023, ambalo linatanguliza mazungumzo na kuakisi roho ambayo pande zote mbili inatafuta katika kudumisha uhusiano wa Uturuki na Ugiriki.
Comments
No comments Yet
Comment