Dollar

40,4256

0.06 %

Euro

47,3475

0 %

Gram Gold

4.410,8500

-0.01 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais Mwinyi amewahakikishia wananchi kuwa kuwa serikali yake itaendelea kufanya juhudi za kuleta mageuzi katika kuimarisha sekta ya afya.

Rais wa Zanzibar apongeza mchango wa kambi za matibabu

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na kambi za matibabu na uchunguzi wa afya.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Julai 21, 2025, alipoifungua Kambi ya Matibabu ya Kumbukumbu ya Hayati Ali Hassan Mwinyi, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, na kuongezea kusema kuwa kambi hizo zinaisaidia Serikali kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Aidha, Rais Mwinyi amewashukuru madaktari bingwa kutoka Kenya na Marekani kwa uamuzi wao wa kuja Zanzibar na kushirikiana na madaktari wazalendo kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Wakati huo huo, Rais Mwinyi amewahakikishia wananchi kuwa kuwa serikali yake itaendelea kufanya juhudi za kuleta mageuzi katika kuimarisha sekta ya afya.

Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuimarisha majengo na miundombinu ya sekta ya afya, kuongeza wataalamu wabobezi, pamoja na kuimarisha maslahi yao.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#