Dollar

38,5694

0.32 %

Euro

43,6893

0.3 %

Gram Gold

4.005,7600

0.04 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Polisi nchini Kenya wanasema mauaji ya kiongozi huyo 'yalipangwa na yalikuwa mahsusi'

Rais Ruto ataka uchunguzi wa kina kufanyika kuhusu mauaji ya mbunge Nairobi

Rais William Ruto ametoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya mbunge Charles Ong’ondo Were aliyeuawa Jumatano usiku na waliohusika kuwajibishwa kisheria.

Alitoa salamu zake za rambirambi kupitia mtandao wa X akisema ‘‘Mungu aifariji familia na awape nguvu watu wa Kasipul kutokana na kifo cha Mheshimiwa Charles Ong’ondo Were’’, alisema Ruto. ‘‘Tunatoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo. Na wale waliohusika kuwajibishwa,’’ aliongeza.

Polisi nchini Kenya wanasema mbunge huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana ambaye alikuwa kwenye pikipiki katika mji mkuu, Nairobi Jumatano usiku. Polisi waliongeza kuwa mauaji hayo yanaonekana kupangwa na yenye lengo mahsusi.

Charles Were, anayewakilisha eneo bunge la Kasipul lililoko magharibi mwa Kenya, alipigwa risasi na kuuawa saa moja na nusu usiku wakati gari lake liliposimama kusubiri taa kwenye barabara ya Ngong, polisi walisema kwenye taarifa waliyoitoa siku ya Jumatano.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#