Sport
Dollar
38,5992
0.33 %Euro
43,6545
0.2 %Gram Gold
4.017,2800
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kuna visa vya mara kwa mara za raia wa Ethiopia kuingia Afrika Kusini kwa njia zisizo halali hasa kupitia mawakala.
Polisi wa Afrika Kusini walitangaza kuwa wamewaokoa raia 44 wa Ethiopia ambao wanadaiwa kuzuiliwa katika eneo tajiri la Johannesburg.
Inaripotiwa kwamba, 17 kati yao ni watoto wadogo.
Kundi hilo liligunduliwa katika nyumba moja huko Sandton, mojawapo ya vitongoji tajiri zaidi vya jiji hilo, kufuatia taarifa iliyochochewa na vilio vya kuomba msaada.
Maafisa waliokuwa doria walijibu na kuwakuta waathiriwa wakiwa wamejifungia ndani ya vyumba kadhaa, kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi Luteni Kanali Mavela Masondo.
"Tulikuta wahamiaji haramu 44 wakiwa wamefungiwa vyumbani, na 17 kati yao ni watoto wadogo," Masondo aliviambia vyombo vya habari.
Maafisa walishtushwa na vilio vya kuomba msaada kutoka kwa nyumba hiyo, na kusababisha ugunduzi huo mbaya.
"Tuligundua kuwa kulikuwa na wahamiaji haramu waliokuwa wamefungiwa vyumbani," alisema Masondo.
Alidokeza kuwa mamlaka ilikuwa ikingoja kuwasili kwa wakalimani ili kuwasiliana vyema na watu waliookolewa na kukusanya taarifa zaidi.
Kesi hii ni ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa matukio ya biashara haramu ya binadamu nchini Afrika Kusini, ambayo mara nyingi hutazamwa kama lango la wahamiaji wasio na vibali kutoka bara zima la Afrika.
Mwezi Machi, polisi waliwaokoa Waethiopia 32 - wengi wao wakiwa watoto na vijana -baada ya kuripotiwa kutoroka utumwani katika kitongoji cha Johannesburg.
Bado haijafahamika iwapo matukio hayo mawili yanahusiana.
Washukiwa watatu walikamatwa Alhamisi usiku, na bunduki haramu ilipatikana katika eneo la tukio.
Polisi wanasema bado wanajaribu kukusanya taarifa zaidi kutoka kwa waathiriwa kwa usaidizi wa wakalimani.
Kesi hiyo inaongeza msururu wa matukio kama hayo kote Johannesburg, ambapo wahamiaji kutoka Ethiopia, wengi wao wakikimbia umaskini na ukosefu wa ajira, wanatumiwa na mitandao ya magendo.
Mnamo Januari 2025, Waethiopia 26 waliokolewa kutoka katika nyumba ambapo walipatikana bila nguo na wakiwa na utapiamlo mkali.
Mnamo Agosti 2024, zaidi ya 80 waligunduliwa wakiwa wamefungiwa ndani ya makazi madogo ya kitongoji, wakiteseka chini ya "hali zisizo za kibinadamu," kulingana na polisi.
Comments
No comments Yet
Comment