Sport
Dollar
38,5992
0.33 %Euro
43,6545
0.2 %Gram Gold
4.017,2800
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mbunge Charles Were aliuawa jioni ya Aprili 30 jijini Nairobi na watu waliokuwa na silaha ambao inaaminika walikuwa wakimfuatilia, huku taarifa sasa zikisema kuwa alipigwa risasi nne.
Maafisa wa upelelezi wa mauaji kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Kenya wanasema wamepiga hatua katika uchunguzi wa mauaji ya Mbunge wa eneo la Kasipul, lililoko magharibi mwa Kenya, Charles Were.
Were aliuawa jioni ya Jumatano, Aprili 30, kwenye Barabara ya Ngong, karibu na eneo la Hifadhi ya Maiti ya Jiji na watu waliokuwa na silaha ambao inaaminika walikuwa wakimfuatilia, huku taarifa sasa zikisema kuwa alipigwa risasi nne.
Hata wakati wapelelezi wakiendelea kutumia teknolojia kumtambua mtu anayeaminika kuwa mshukiwa mkuu wa mauaji ya Were, picha za CCTV zilizopatikana na polisi zinatarajiwa kumbaini mshukiwa aliyetekeleza mauaji hayo.
Mbali na kutegemea picha za CCTV, maafisa hao wa DCI pia wanazingatia taarifa walizokusanya kutoka kwa dereva na mlinzi wa mbunge huyo katika kuwasaka wauaji.
Inasemekana Were aliondoka kwenye Majengo ya Bunge mwendo wa saa moja jioni akiwa na mlinzi wake na dereva, baada ya muda mfupi dereva huyo akashuka kwenye gari na kuingia kwenye duka la karibu la M-Pesa, ambapo aliweka shilingi za Kenya 20,000 kwa niaba ya bosi wake.

Muda mfupi baadaye, mtu ambaye anaonekana akifuata gari la mbunge huyo alishuka kutoka kwenye pikipiki na kuzunguka gari, akimpiga risasi nne kwa karibu.
Risasi ya kwanza ilivunja dirisha la gari, huku risasi zilizofuata zikipenya kwenye mkono na kifua cha mbunge.
Juhudi za mlinzi wa mbunge huyo kuwafuata washambuliaji hazikufanikiwa.
Kisha mlinzi akaamua kumpeleka mbunge huyo hospitalini, lakini Were alifariki alipowasili katika Hospitali ya Nairobi.
Comments
No comments Yet
Comment