Dollar

38,5992

0.33 %

Euro

43,6545

0.2 %

Gram Gold

4.017,2800

0.33 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Maafisa walikuwa wakiwafuatilia magaidi hao kwa siku mbili kutokana na taarifa za kijasusi kuwa walikuwa wamejificha katika moja ya misitu mikubwa pwani ya Kenya.

Polisi watano wauawa Kenya katika makabiliano na kundi la al-Shabaab

Polisi wasiopungua watano wameuawa nchini Kenya siku ya Jumanne jioni katika makabiliano na wanaoaminika kuwa magaidi wa kundi la al-Shabaab kwenye msitu wa Boni, eneo la Lamu, pwani ya Kenya.

Maafisa wengine wa kikosi maalum walijeruhiwa, polisi wamesema.

Polisi hao walivamiwa wakati wakiwasaka magaidi wa al Shabaab katika msitu huo mkubwa.

Polisi wanaamini kuwa pia wamefanikiwa kuwaua baadhi ya magaidi.

Maafisa waliojeruhiwa walisafirishwa hadi mjini Nairobi kwa matibabu zaidi.

Waziri wa Mambo ya ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen aliwatembelea maafisa waliojeruhiwa hospitali siku ya Alhamisi.

“Maafisa wetu wa usalama wamejitolea sana kuhakikisha tuko salama na wanahitaji tuwaunge mkono katika hili,” waziri Murkomen alisema, akiwa ameandamana na Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja, na Manaibu Inspekta Jenerali Eliud Lagat na Gilbert Masengeli, miongoni mwa maafisa wengine wakuu wa polisi.

Haya ni mashambulio ya hivi karibuni kufanyika huku operesheni ya kuwakabili magaidi hao zikiendelea.

Maafisa kutoka vitengo mbalimbali wako katika eneo hilo kuwakabili wapiganaji huku mashambulizi yakiendelea.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#