Sport
Dollar
38,5684
0.33 %Euro
43,8996
0.79 %Gram Gold
4.040,8700
0.92 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, kimeta ni ugonjwa wa mlipuko utokanao na vimelea vya bakteria vinavyojulikana kitaalamu kwa jina la ‘bacillus anthracis’.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imethibitisha mlipuko wa ugonjwa wa Kimeta nchini humo huku mtu mmoja akipoteza maisha.
Mlipuko huo umeripotiwa katika eneo la jimbo la Kivu ya Kaskazini, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Ugonjwa huo unadaiwa kuathiri kanda nne za kiafya karibu na ziwa Edward kwenye mpaka na nchi ya Uganda.
Tahadhari za mapema kuhusu uwepo wa ugonjwa huo zilitolewa Machi 22, 2025 kufuatia taarifa za vifo vya viboko na nyati, ndani ya hifadhi ya Virunga iliyopo nchini DRC.
“Jitihada zetu zililenga kupunguza maambukizi toka kwa wanyama hadi kwa binadamu. Kwa sasa, tunafanya kazi kwa ukaribu na serikali, jamii za wadau wengine wa maendeleo ili kuongeza na kulinda afya ya umma,” amesema Boureima Sambo, mwakilishi wa WHO nchini DRC katika taarifa yake.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, kimeta ni ugonjwa wa mlipuko utokanao na vimelea vya bakteria vinavyojulikana kitaalamu kwa jina la ‘bacillus anthracis’.
Ni ugonjwa unaowakumbuka wanyama na unaweza kuambukizwa kwa binadamu kupitia kula na kunywa nyama na maziwa ya mnyama aliyeathirika au hata kumgusa.
Comments
No comments Yet
Comment