Mashindano ya soka la ufukweni yanaanza Jumamosi tarhe 28 Novemba, katika eneo la pwani la Saly.

NEWSTIMETR
NEWSTIMETR
Morocco, Senegal huenda wakakabiliana tena katika Soka la Ufukweni la CAF

Morocco and Senegal huenda wakakabiliana tena wakati mataifa hayo mawili yanapojiandaa kwa michuano ya Soka la Ufukweni ya CAF nchini Senegal, siku chache baada ya uamuzi muhimu uliowarudishia Senegal kombe lao la AFCON 2025.

Mashindano ya soka la ufukweni yanaanza Jumamosi, tarehe 28 Novemba katika eneo la pwani la Saly, huku Senegal wakitafuta ubingwa wa taji hilo kwa mara ya sita mfululizo na Morocco wakitaka kulinyanyua kwa mara ya kwanza.

Pande zote mbili ziko katika makundi tofauti, kumaanisha hawawezi kukutana katika hatua ya kwanza. Lakini kama wote watamaliza miongoni mwa timu mbili bora katika makundi yao, wanaweza wakapambana katika nusu fainali tarehe 4 Disemba au katika fainali siku mbili baadaye.

Uwezekano wa kukabiliana unakuja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) siku ya Jumanne tarehe 24, Novemba, kubatilisha uamuzi wa Bodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka barani Afrika ambao ulikuwa umewapokonya Senegal ushindi wa AFCON 2025 na kuwapa Morocco ushindi wa magoli 3-0.

Wenyeji Senegal, na mabingwa watetezi, wako kwenye Kundi A pamoja na Msumbiji, Uganda na Ghana. Morocco wako Kundi B pamoja na Mauritania, Malawi na Angola.

Senegal ndiyo wababe wa michuano hii ya ufukweni, ambapo wameshinda mara tano 2016, 2018, 2021, 2022 na 2024. Morocco, nao, wamemaliza katika nafasi ya tatu kwenye mashindano matatu yaliyopita mfululizo na wanatarajia kuwa hii itakuwa nafasi yao ya ushindi kwa mara ya kwanza.

Michuano hiyo pia ni nafasi ya Afrika kufuzu kwa Soka la Ufukweni Kombe la Dunia FIFA 2027, ambapo timu zitakazocheza fainali zinafuzu moja kwa moja.

TRT Afrika Swahili — TRT Afrika Swahili

#