Rais wa CAF Patrice Motsepe ametangaza hatua hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 48 wa CAF uliofanyika Jijini Abuja, Nigeria.

Kiswahili sasa lugha rasmi CAF

Shirikisho la Mpira Barani Afrika (CAF) limeidhinisha Lugha ya Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi za shirikisho hilo baada ya kufanya mabadiliko madogo katika Katiba ya CAF.

Rais wa CAF Patrice Motsepe ametangaza hatua hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 48 wa CAF uliofanyika Jijini Abuja, Nigeria.

Kufuatia uamuzi huo, Kiswahili kinaungana na lugha nyingine nne ambazo Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu na Kireno kuwa lugha rasmi zinazotumika katika shughuli za CAF ikiwemo mikutano na matukio mbalimbali yanayoandaliwa na CAF.

Akitangaza uamuzi huo, Motsepe ameipongeza Tanzania, Kenya na Uganda kwa kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya CAF na kwamba anaamini hiyo ni fursa muhimu kwa Afrika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari nchini Tanzania ambae pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Tanzania na Afrika Mashariki imepokea uamuzi huo wa CAF kwa heshima kubwa na itahakikisha inatumia fursa hiyo ipasavyo kukuza lugha hiyo ambayo ina wazungumzaji takriban milioni 500 duniani kote.

TRT Afrika — TRT Afrika

Picha: AFP (Wire)

#