Kadogosa ametoa maelekezo hayo alipokuwa Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya miundombinu ya Barabara ya Tanga - Pangani Pamoja na Daraja la Pangani.
Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania Masanja Kadogosa, ameagiza kusimamishiwa usajili wa aliyekuwa Mhandisi Mshauri (Doch Limited) wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Tanga - Pangani yenye urefu wa kilomit 50 ambayo imeanza kupata nyufa kabla ya kukamilika.
Wakati huo huo, ameiagiza Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kufanya uchunguzi wa kina kuhusu utendaji wa Mhandisi Mshauri huyo, ili kubaini iwapo kulikuwa na uzembe au ukiukwaji wa maadili ya taaluma katika usimamizi wa mradi huo.
Waziri Kadogosa pia ameelekeza Wizara ya Ujenzi kuunda timu maalumu ya uchunguzi itakayowasilisha taarifa ndani ya siku saba ili kubaini sababu za barabara hiyo kuanza kuharibika ndani ya kipindi kifupi, pamoja na uwajibikaji wa wataalamu waliosimamia utekelezaji wa mradi huo, hususan katika kuhakikisha ubora wa vifaa vilivyotumika na kazi zilizofanyika unakidhi viwango vilivyowekwa.
Kadogosa ametoa maelekezo hayo alipokuwa Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya miundombinu ya Barabara ya Tanga - Pangani Pamoja na Daraja la Pangani.
TRT Afrika — TRT Afrika
Afrika
