Waziri wa mambo ya nje anatoa wito kwa mashirikisho ya kimataifa ya michezo kubatilisha uamuzi huo, akisema kuwa kuna hatari ya kuhalalisha vita vya Urusi dhidi ya Ukraine

Ukraine yapinga uamuzi wa kuipa Moscow uwenyeji wa Mashindano ya kunyanyua vyuma 2030

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha siku ya Jumatatu aliutaja uamuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Kunyanyua Vyuma (IWF) kuupa mji wa Moscow uwenyeji wa Mashindano ya Dunia 2030 "usiokubalika."

Katika mtandao wa kijamii wa Marekani X, Sybiha alisema uamuzi huo, ambao umefanyika tangu kuanza kwa vita vya Urusi na Ukraine hauko sawa, na kuna hatari ya kurudi kwa mashindano ya kimataifa nchini Urusi kuonekane kama jambo la kawaida.

"Urusi inaendelea kuwaua watu wa Ukraine, ikiwemo wanamichezo. Ni kinyume na maadili kuwapa uwenyeji Moscow wa mashindano ya michezo ya kimataifa wakati wakiendeleza mashambulizi," alisema.

Sybiha anataka IWF, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na mashirika ya michezo ya kimataifa kushirikiana kwa lengo la kubatilisha uamuzi huo, akisisitiza kuwa "pale mashirika ya michezo kimataifa yanapofumbia macho washambuliaji, inapoteza heshima ya kukemea kuhusu haki, heshima na uadilifu."

Mwezi Julai, IOC iliondoa kwa muda marufuku ya Kamati ya Olimpiki ya Urusi, ikiashiria kuwapa nafasi wanamichezo wa Urusi kushiriki Olimpiki ya 2028 huko Los Angeles.

Mara ya mwisho kwa jiji la Moscow kuwa wenyeji wa Mashindano ya Kunyanyua Vyuma ilikuwa mwaka 1983.

#