Michuano hiyo itakuwa na timu 19 kutoka mashirikisho 6, huku Arsenal, Barcelona zikiwa miongoni mwa vilabu 7 ambavyo vimeshafuzu

Marekani mwenyeji wa mashindano ya kwanza ya Wanawake Kombe la Dunia la Klabu FIFA 2028

Marekani itakuwa mwenyeji wa mashindano ya kwanza ya Wanawake Kombe la Dunia la Klabu FIFA kuanzia Januari 5 hadi 30, 2028, timu 19 zikishiriki kutoka mashirikisho sita ya soka, FIFA ilitangaza siku ya Alhamisi.

FIFA ilisema kuwa Marekani iliteuliwa kutokana na uzoefu wake wa kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa, miundombinu mizuri ya michezo na hamasa ya soka la wanawake.

"Kwa Marekani' kuwa wenyeji wa michuano iliofanikiwa ya FIFA hivi karibuni, pamoja na kuonesha hamasa kwa soka la wanawake ukijumuisha miundombinu ya michezo, imefanya nchi hiyo kuwa bora," Mkuu wa Soka la Wanawake FIFA Sarai Bareman alisema.

FIFA pia ilithibitisha vilabu saba ambavyo tayari vimeshafuzu: Arsenal (England), Barcelona (Hispania), Club America (Mexico), Gotham FC (Marekani), Naegohyang (Korea Kaskazini), Corinthians (Brazil) na Wuhan Jiangda (China).

Nafasi zingine 12 zilizobaki zitajazwa kwa njia ya mashindano ya mabara, huku vipaumbele vikipewa mabingwa wa ligi kati ya 2024 na 2027.

Ulaya itawakilishwa na timu sita, huku Asia, Afrika, Kaskazini na Marekani ya Kati na Karibi, na Marekani Kusini ikipata wawakilishi watatu kila mmoja. Oceania itawakilishwa na timu moja.

Mashindano hayo yatafanyika baada ya kila miaka minne ikiwa ni sehemu ya juhudi za FIFA za kuimarisha soka la wanawake la klabu.

#