Afrika Mashariki, Kenya inaongoza, ikifuatiwa na Uganda, baadae Tanzania.

Tanzania miongoni mwa nchi 10 Afrika zenye ufasaha wa lugha ya Kiingereza

Tanzania imekuwa katika orodha ya kumi bora ya nchi zenye ufasaha wa lugha ya Kiingereza Afrika kwa mwaka 2026. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya kimataifa ya kila mwaka inayopima kiwango cha umahiri wa lugha ya Kiingereza miongoni mwa watu wazima katika kila nchi iliyofanywa na Education First.

Kwa mujibuwa ripoti hiyo, Tanzania imepata alama 477, na kushika nafasi ya 70 duniani.

Afrika Mashariki, Kenya inaongoza, ikifuatiwa na Uganda, baadae Tanzania.

Afrika Kusini ndiyo iliyoibuka kidedea Afrika kwa alama 588, ikichuana na Zimbabwe yenye alama 587 na Kenya yenye alama 582.

Nchi nyengine zilizoingia katika orodha hiyo ni pamoja na Nigeria, Ghana, Ethiopia, Morocco na Tunisia.

TRT Afrika — TRT Afrika

Picha: TRT Afrika Swahili

#