Gharama hiyo inajumuisha operesheni za kijeshi, matumizi ya silaha na risasi, pamoja na gharama za kubadilisha vifaa vya kijeshi vilivyotumika au kuharibiwa.

Vita dhidi ya Iran vyaigharimu Marekani zaidi ya Dola bilioni 48

Vita vya Marekani dhidi ya Iran vimeigharimu Marekani kiasi kinachokadiriwa kufikia Dola bilioni 48.3 tangu vilipoanza mwishoni mwa mwezi Februari. Hayo yalielezwa na afisa wa bajeti wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani alipokuwa akitoa ushahidi mbele ya wabunge tarehe 19 Novemba.

Kiasi hicho kinajumuisha gharama za operesheni za kijeshi, silaha na risasi zilizotumika, pamoja na vifaa vya kijeshi vilivyohitaji kubadilishwa. Hata hivyo, kiasi hicho hakijumuishi gharama za ukarabati wa kambi na miundombinu ya kijeshi ya Marekani katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati iliyoharibiwa na mashambulizi ya Iran.

Afisa huyo wa bajeti wa Pentagon, Arthur Miller, alisema kuwa hakuweza kutoa makadirio ya gharama za ziada za ukarabati. Hata hivyo, taarifa zilizoripotiwa zinaeleza kuwa gharama hizo tayari zinafikia mabilioni ya dola.

Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran Februari 28, huku mapigano yakipungua baadaye, kufuatiwa na makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi Aprili.

Hata hivyo, uhasama ulianza tena baada ya mazungumzo ya pande hizo kukwama, licha ya kuwa nchi hizo mbili zilikuwa zimesaini hati ya makubaliano ya maelewano mwezi Juni.

TRT Afrika — TRT Afrika

Picha: Reuters

#