Kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, Erdogan amesema kuwa, ni vyema kuwa kiongozi ajaye wa Umoja wa Mataifa abebe maono na uzoefu unaohitajika, katika kurudisha hadhi ya umoja huo.
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na Emmanuel Macron wamejadiliana masuala mbalimbali, ikiwemo mahusiano ya nchi zao, huku Erdogan akitoa wito wa kuwepo na uongozi imara ndani ya Umoja wa Mataifa.
Kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, Erdogan amesema kuwa, ni vyema kuwa kiongozi ajaye wa Umoja wa Mataifa abebe maono na uzoefu unaohitajika, katika kurudisha hadhi ya umoja huo.
Atagaza mageuzi ndani ya Umoja wa Mataifa
Kauli ya Erdogan ni msisitizo wa Uturuki, wenye kutaka kuona uongozi utakaoweza kutatua changamoto za kiulimwengu, ndani ya Umoja wa Mataifa.
Amkaribisha Macron kwa ajili ya Mkutano wa COP31
Wakati wa mazungumzo hayo, Erdogan alimkaribisha Macron kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Nchi Duniani, ambao unaandaliwa na Uturuki.
Kwa upande wake, Macron alimpongeza Rais Erdogan kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Jamhuri.
