Ukiwa na kauli mbiu isemayo, “ Umoja katika Lugha, Mawazo na Matendo, mkutano huo unaandaliwa na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki.

Biashara, ushirikiano wa anga kuwa sehemu ya ajenda ya mkutano wa nchi za Kiturki

Uturuki inaandaa mkutano wa 13 wa Umoja wa nchi za Kiturki (OTS) utakaofanyika Alhamisi na Ijumaa, kutathimini maendeleo ya ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji, nishati na miundombinu ya kidijiti.

Ukiwa na kauli mbiu isemayo, “ Umoja katika Lugha, Mawazo na Matendo, mkutano huo unaandaliwa na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki.

Wakati wa mkutano huo, Uturuki itachukua nafasi ya urais wa OTS kutoka Azerbaijan, ambapo washiriki wanatarajiwa kupitisha azimio la Ankara, na makubaliano yenye kulenga kukuza uhusiano.

Ushirikiano katika sekta ya kidijiti itakuwa ni kati ya ajenda zitakazotawala mkutano, ambapo Uturuki itakuwa nchi ya tatu baada ya Azerbaijan na Uzbekistan kupitisha ushirikiano wa uchumi wa kidijiti.

Kuelekea mkutano huo, Umoja wa Wafanyabiashara wa Uturuki (TOBB) wataandaa jukwaa la kibiashara la Kiturki, ambalo litaangazia ushoroba wa kati na masuala ya forodha.

Rais wa Turkmenistan, Serdar Berdimuhamedow anatarajia kukutana na umoja wa wafanyabiashara wa Uturuki, siku ya Ijumaa.

 

#