Akizungumza na wanahabari mara baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri jijini Ankara siku ya Jumatatu, Erdogan alisema kuwa Uturuki haikuwa na lengo la kuzizunguka nchi zingine, bali ilikuwa na nia ya kulinda maslahi yake.
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesisitiza utayari wa Uturuki katika kulinda na kutetea maslahi yake ya bahari na eneo zima la Mashariki mwa Mediterenia, akitoa wito wa kuheshimu nia ya pamoja ya Uturuki na Libya ya kumaliza mgawanyiko katika taifa hilo la Afrika Kaskazini.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri jijini Ankara siku ya Jumatatu, Erdogan alisema kuwa Uturuki haikuwa na lengo la kuzizunguka nchi zingine, bali ilikuwa na nia ya kulinda maslahi yake.
Kulingana na Erdogan, sera ya Mambo ya Nje ya Uturuki, imeegemea maslahi ya nchi, akiweka bayana kuwa, Uturuki haitosita kuchukua hatua stahiki kwa gharama yoyote ile.
Erdogan atoa wito wa umoja na majadiliano ya Libya
Erodgan alisema kuwa, Uturuki inaamini kuwa umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu za kupata amani, ustawi, na usalama, akiongeza kuwa, Uturuki inaendeleza jitihada za kupunguza migogoro na kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
“Uturuki isingependa kuona mwagwanyiko ndani ya Libya, au ndani ya nchi yeyote ya Kiislamu,” alisema.
Uturuki yasisitiza msimamo wake wa Mashariki ya Mediterinea
Kauli ya Erdogan, ilionesha msimamo wa Uturuki katika suala la haki za bahari, akisisitiza kuwa ni vyema kwa haki hizo kuheshimiwa licha ya uwepo wa migogoro ya kikanda.
Mara kwa mara, Uturuki imetetea ushirikiano wake na Libya, ikiwemo mikataba ihusuyo sheria za majini.
Akizungumzia mkutano ujao wa 13 wa umoja wa nchi za Kiturki, Erdogan aliweka msisitizo kwenye umuhimu wa umoja kati ya mataifa hayo.
"Kama jumuiya ya Kiturki, ni imani yangu kuwa, kwa mara nyingine tena, tutasimama pamoja kwa umoja na mshikamano, dhidi ya wale wenye lengo la kudharau umoja wetu,” alisema.
Akizungumzia migogoro ya kikanda, Erdogan alisema kuwa Uturuki inaendelea kumaliza vurugu na umwagaji damu.
"Sisi kama Uturuki, tunajitahidi, kadiri ya uwezo wetu, kumaliza mateso na umwagaji damu," aliongeza.

