Muswada huo, uliidhinishwa siku ya Jumanne, baada Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Levent Gumrukcu kujibu maswali ya wabunge wengine.

Bunge la Uturuki lauidhinisha mkataba wa Makkah

Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Uturuki, imeidhinisha muswada wa kupitisha mkataba wa ulinzi wa Makkah, unaohusisha nchi za Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan.

Muswada huo, uliidhinishwa siku ya Jumanne, baada Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Levent Gumrukcu kujibu maswali ya wabunge wengine.

Akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo, Gumrukcu alisema kuwa, mkataba huo unalenga kuimarisha usalama wa kikanda kupitia ushirikiano.

“Mkataba huu ni jambo muhimu kwa kanda yetu,” alisema Gumrukcu.

Kulingana na Gumrukcu, Saudi Arabia na Pakistan, tayari zimemaliza mchakato wa kupitisha mkataba huo ndani ya nchi zao.

Aliongeza kuwa, mkataba huo utakuwa ni hatua muhimu ya kuanzisha sera ya ulinzi wa kikanda.

Kulingana na Naibu Waziri huyo, mkataba huo haulengi tu nchi washirika, bali ukanda mzima.

Mkataba wenye ‘kukuza mtangamano’

Alisisitiza kuwa, mkataba huo wa kiulinzi, haukuwa na lengo la kuishambulia nchi yoyote, akiongeza kuwa upo wazi kwa mataifa yote ya kikanda yenye kuheshimu sheria za kimataifa, ikiwemo utatuzi wa migogoro.

“Mkataba huu ni shirikishi na unalenga kukuza mtangamano,” alisema.

Alisisitiza kuwa, mkataba huo, hautoshusha hadhi ya majukumu ya Uturuki na washirika wake.

Aliongeza kuwa, mkataba huo, utafikisha azma ya Uturuki ya kushiriki kwenye majukwaa makubwa, hususani NATO, katika kuchangia katika usalama na utulivu wa Mashariki ya Kati.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Fuat Oktay, alipuuzia madai kuwa mkataba huo utakuwa ni mbadala wa NATO.

“Kulikuwa na maswali kuwa, iwapo mkataba huu utakuwa mbadala wa NATO, hilo jambo si kweli,” alisema Oktay.

#