Mashindano hayo yatafanyika kuanzia tarehe 19 Juni hadi 17 Julai, 2027.

Tanzania yapewa miji 3 kuandaa AFCON 2027, Uganda 2, Kenya 1

Tanzania imepata nafasi ya kuongoza kwa idadi ya miji itakayotumika kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027, baada ya kutengewa miji mitatu kati ya sita itakayotumika katika mashindano hayo.

Miji ya Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar ndiyo itakayoiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo, huku Uganda ikipata miji miwili ambayo ni Kampala na Hoima.

Kwa upande wa Kenya, itakuwa na mji mmoja pekee wa Nairobi kwa ajili ya kuandaa michezo ya AFCON 2027.

Mgawanyo huo unaifanya Tanzania kuwa na asilimia 50 ya miji yote sita ya mwenyeji, Uganda asilimia 33.3 na Kenya asilimia 16.7.

Michuano hiyo ya AFCON 2027 itaandaliwa kwa ushirikiano wa nchi hizo tatu za Afrika Mashariki, katika kile kinachotajwa kuwa fursa muhimu ya kukuza soka, utalii na uchumi wa ukanda huo.

Mashindano hayo yatafanyika kuanzia tarehe 19 Juni hadi 17 Julai, 2027.

TRT Afrika — TRT Afrika

Picha: Wengine

#