Paul Mackenzie anatumikia kifungo cha miaka 200 kwa mauaji ya watoto takriban 200 kwa njaa
Kiongozi wa dhehebu tata la Good News International Ministries nchini Kenya, Paul Mackenzie, anayetumikia kifungo cha miaka 200 kwa mauaji ya watoto takriban 200 kwa njaa, amehukumiwa kwa mashtaka mapya ikiwemo ukatili kwa watoto na kushambulia watu katika mauaji hayo ya halaiki.
Hakimu katika Mahakama ya Watoto ya Tononoka huko Mombasa alitoa uamuzi kwamba Mackenzie alikuwa amewashauri wazazi katika jamii ya Shakahola kuwauwa watoto wao kwa kuwanyima chakula.
"Mahakama imebaini kuwa huko Shakahola... mshtakiwa wa kwanza (Mackenzie) aliwashawishi wote waliokuwepo hapo wafunge hadi wafe, na kwamba watoto waanze, wakifuatiwa na wanawake, na hatimaye wanaume," alisema hakimu Nelly Chepchirchir.
Alimhukumu kwa makosa matano ya ukatili kwa mtoto na kosa moja la kushambulia na kusababisha madhara halisi ya mwili.
Mackenzie aliongoza kanisa katika msitu karibu na pwani ya Kenya.
Waathiriwa wake wanaoshukiwa 500 ni pamoja na watoto waliozikwa wakiwa hai au kutupwa kwenye vyoo, katika mojawapo ya mauaji ya halaiki yaliyosababisha vifo vingi zaidi yatokanayo na imani tata za dini.
Mapema mwezi huu, Mackenzie alihukumiwa kifungo cha miaka 100 jela kwa mauaji ya njaa na miaka 100 kwa mauaji ya moja kwa moja.
Mackenzie alikana mashtaka yaliyokuwa yakimkabili na atahukumiwa baadaye.
Mackenzie bado anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi, uenezi wa itikadi kali, na mauaji ya watu wengi katika kesi zijazo mahakamani.
TRT Afrika / Reuters (Wire) — TRT Afrika / Reuters (Wire)
Picha: Reuters (Wire)

