Picha kutoka kwa eneo la tukio zinaonesha moto na moshi mweusi katika wingu la eneo lenye watu wengi la Al-Waraq.
Waendesha mashtaka wa Misri wametangaza siku ya Alhamisi kuwa wamemkamata mtu mmoja kwa kusababisha moto mkubwa baada ya lori la mafuta kupinduka katika barabara kuu jijini Cairo, na kusababisha vifo vya watu 31.
Waendesha mashtaka wanasema mtu huyo “alikiri” kuendesha kwa kasi wakati gari lake lilipogongana na lori la mafuta, “kusababisha usukani kuteleza mikononi mwake na gari lake kwenda pembeni”.
Wakati gari hilo lilipogongana na lori, moja ya tairi lake lililipuka, kusababisha gari kupinduka, waendesha mashtaka walisema. Moto ulizuka kutokana na petroli kuvuja, waliongeza.
Picha kutoka kwa eneo la tukio zinaonesha moto na moshi mweusi katika wingu la eneo lenye watu wengi la Al-Waraq huku waendesha magari waliokuwa kwenye barabara hiyo kuu wakipiga honi zao na kujaribu kuondoka eneo la ajali.
TRT Afrika Swahili — TRT Afrika Swahili
Picha: َAA
