Akizungumza siku ya Alhamisi, Fidan alisisitiza kuwa, mkataba huo hauhalalishi mashambulizi dhidi ya nchi nyingine.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan amesema kuwa nchi yake imekamilisha mkataba wa amani wa Makkah, tayari kupelekwa bungeni kuidhinishwa.
Akizungumza siku ya Alhamisi, Fidan alisisitiza kuwa, mkataba huo hauhalalishi mashambulizi dhidi ya nchi nyingine.
“Mkataba huo umekamilika, na upo tayari kupelekwa bungeni,” alisema Fidan wakati wa mkutano wa waandishi wa habari, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungaria, Anita Orban.
Fidan alisisitiza kuwa, mkataba huo, unazitaka nchi husika, kutoa msaada kwa nchi nyingine inapokabiliwa na shambulizi la aina yoyote.
“Huu si mkataba wa kushambulia wengine, unalenga kutoa msaada kwa mwenzetu anapopatwa na matatizo,” alisema.
Hali kadhalika, Fidan alisisitiza kuwa, mkataba huo hauipi Uturuki mamlaka ya kutuma vikosi vyake kwa ajili ya kufanya uvamizi.
Mkataba huo, ulisainiwa Agosti 7 jijini Makkah, na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, na Mwanamfalme wa Saudi Arabia.
Mbali na kuonesha utayari wa nchi hizo tatu katika kutafuta suluhu ya migogoro ya kikanda, mkataba huo pia unalenga kuimarisha uwezo wa hizo kiulinzi.
Wakati huo huo, Fidan alitahadharisha kuhusu kuruhusu mgogoro kati ya Urusi na Ukraine kufika katika eneo la Bahari Nyeusi.
“Tusikubali kuigeuza Bahari Nyeusi kuwa sehemu nyingine ya mgogoro,” aliongeza.

