Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema serikali yake bado ina dhamira ya kuwa na mchakato wa "Uturuki isiyo na Ugaidi", akiahidi kuendeleza hilo kwa makubaliano ya kisiasa na kijamii.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema Uturuki inaendelea na dhamira yake ya kuimarisha uchumi, uhuru wa sekta ya ulinzi, na mchakato wa “Uturuki isiyo na Ugaidi”, akisisitiza umuhimu wa makubaliano ya kisiasa na kijamii.
“Serikali yetu inadhamiria kukuza uchumi wa Uturuki, sekta yake, chakula chetu, mkate wetu, amani yetu na mafanikio,” Erdogan alisema baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri katika Ikulu ya Rais jijini Ankara siku ya Jumatatu.
“Tuko imara katika utekelezaji wa ukuaji wetu kimkakati kwa kuzingatia uwekezaji, uzalishaji, ajira na kuuza bidhaa nje ya nchi,” aliongeza.
Rais alisema kuwa lengo la Uturuki ni kuwa na sekta huru ya ulinzi, akiahidi kuendelea kufanya kazi “bila kusita, bila kupumzika na, muhimu zaidi, bila kufikiria kuhusu wale wasio na dira.”
Akieleza kuhusu miradi ya sekta ya ulinzi ya KIZILELMA na EJDERHA, Erdogan alisema: “Huu ni mwanzo tu. Mungu akipenda, tutatengeneza za kisasa na zenye uthabiti zaidi.”
‘Uturuki isiyo na Ugaidi’
Kuhusu mchakato wa “Uturuki isiyo na Ugaidi”, Erdogan anasema kuimarisha usalama kunasaidia kuondoa vikwazo kwa uwekezaji, uzalishaji, ajira, na utalii.
Anasema mapango 14 zaidi huko Hakurk, karibu na mpaka wa Uturuki—ambayo kwa muda mrefu yamekuwa maficho ya magaidi—yameondolewa kwenye hatari, kufanya mapango karibu yote ya kanda ya Hakurk kaskazini mwa Iraq, Zap na Metina kukaribia kuwa salama kabisa.
“Huku hali ya usalama ikiendelea kuimarika katika kanda hiyo, vikwazo kwa uwekezaji, uzalishaji, ajira na utalii vinaondolewa moja baada ya kingine,” alisema.
Erdogan alisisitiza kuwa Uturuki na raia wake “haiwezi kukubali kupoteza. Mashariki na kusini mashariki (maeneo ya mpakani) hayawezi kukosa usalama. Hakuna raia wangu yoyote anayetaka kupoteza tena.”
“Licha ya asili yake, taifa hili halitaki kupoteza tena. Muungano wa (Watu) na serikali unajitahidi kutimiza hili,” aliongeza.
Alisema serikali ina dhamira kwa mchakato huo, akisisitiza jukumu lake na dhamira ya kuhakikisha hilo linafanikiwa.
“Tunafahamu kuhusu jukumu mlilonikabidhi. Tumeweka mioyo yetu, roho zetu, na miili yetu katika kuhakikisha mchakato huu unafanikiwa,” Erdogan alisema.
Mpango wa ‘467’
Aliongeza kutatua masuala kutakuwa rahisi iwapo silaha na vurugu zitaondolewa katika jambo hilo, wakati serikali ikielekeza umuhimu wa kuendeleza mpango wa “467,” akiuita hatua muhimu katika siasa za Uturuki.
Nambari 467 inazungumzia makubaliano ya pamoja ya bunge kutokana na kura 467 zilizopigwa kuunga mkono sheria inayohusiana na mchakato wa “Uturuki isiyo na Ugaidi”.
“Tuna lengo la kuendeleza mchakato wa kuwa na Uturuki isiyo na Ugaidi kwa uwezekano wa makubaliano ya pamoja ya kisiasa na kijamii. Lakini hatutoruhusu suala hili ligeuzwe na kuwa kurubuni kisiasa,” alisema.
Erdogan aliahidi kuendeleza mchakato huo bila kusita, akisema: “Tutaendelea bila kurudi nyuma hata hatua moja na, Mungu akipenda, na kuondoa suala hilo katika taifa letu kabisa.”
TRT Afrika / َAA — TRT Afrika / َAA
Picha: َAA

