Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mafuriko nchini humo yameua watu wapatao 40, na kuwaacha wengine bila makazi
Serikali ya Malawi imeomba msaada wa kimataifa kupambana na janga la mafuriko lililoikumba nchi hiyo.
Kulingana na Idara ya Udhibiti Majanga ya Malawi (DoDMA), watu wapatao 40 nchini humo, wamepoteza maisha, huku maelfu wengine wakikosa makazi.
Mafuriko hayo, pia yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu, ikiwemo barabara ambazo zimetatizo mawasiliano na shughuli za uchukuzi nchini humo.
Kamishna wa DoDMA, Wilson Moleni aliwaambia waandishi wa habari kuwa, “taifa hilo lipo katika hali mbaya kwa sasa.”
“Kama nchi, tumeelemewa nan a mahitaji ya watu walioathirika na mafuriko hayo siku hadi siku. Tayari uchumi wetu umedhoofika. Hatuwezi kutatua tatizo hili sisi wenyewe na ndio maana tunawaomba wadau wetu wa maendeleo kuja kutusaidia,” alisema Moleni.
Mafuriko hayo yanatokea wakati ambapo taifa hilo linakabiliwa na baa la njaa, lililosababishwa na mvua za El Nino, ambazo zimewaacha zaidi ya watu milioni 4.5 wakiwa na mahitaji makubwa ya chakula.
Oktoba mwaka jana, Rais Arthur Peter Mutharika alitangaza hali ya hatari katika wilaya 28, nchini humo, akitoa ombi la msaada wa kibinadamu.
Mwaka 2023, kimbunga kiitwacho Freddy, kiliikumba nchi hiyo, na kuua watu wapatao 1000, na kuwaacha takribani watu milioni 2.5 bila makazi.
Watu 500 bado hawajulikani walipo.
Comments
No comments Yet
Comment