Dollar

43,4293

0.02 %

Euro

52,1720

-0.2 %

Gram Gold

7.315,3500

1.26 %

Quarter Gold

11.952,5300

0 %

Silver

160,7700

2.75 %

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ameahidi kuimarisha ushirikiano na Uturuki katika masuala ya usalama na biashara, akieleza juhudi zao za pamoja kukabiliana na ukosefu wa usalama na kuimarisha ukuaji wa uchumi.

Tinubu wa Nigeria aahidi kushirikiana na Uturuki katika sekta ya usalama, biashara

Kiongozi wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ameahidi kuimarisha ushirikiano na Uturuki katika sekta ya usalama na biashara, akieleza juhudi zao za pamoja kukabiliana na ukosefu wa usalama na kuimarisha ukuaji wa uchumi.

“Nitakuwa pamoja na wewe katika masuala ya demokrasia, uhuru, na maendeleo,” Tinubu alimwambia Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari jijini Ankara siku ya Jumanne.

Wakati wa ziara yake ya kwanza rasmi nchini Uturuki, Tinubu alisema alijadiliana na Erdogan masuala ya maslahi ya pamoja, ikiwemo kuimarisha biashara, kuimarisha fursa za biashara, na kuimarisha uchumi wa pamoja ambao unawawezesha watu wenye nia ya kujifunza na kufanya kazi.

Alisisitiza umuhimu wa mabadiliko ya kiuchumi ambayo yatajumuisha watu ambao wako katika hali mbaya wakati wakiendeleza amani na uthabiti, hasa kote barani Afrika.

Makubaliano tisa muhimu

Kiongozi huyo wa Nigeria alieleza dhamira ya Erdogan kuhusu demokrasia, uhuru, na maendeleo kuwa yenye lengo zuri, hasa kwa kuunga mkono watu ambao wako katika hali mbaya kote duniani.

Alisema juhudi za Uturuki nchini Somalia “zinatambulika.”

Makubaliano tisa yalitiwa saini kati ya Uturuki na Nigeria mbele ya Marais Erdogan na Tinubu kufuatia mazungumzo ya mataifa mawili na kwa ngazi ya ujumbe wa nchi hizo.

Ikijumuisha sekta mbalimbali, makubaliano hayo ni pamoja na ushirikiano katika mafunzo ya kijeshi, sera ya diaspora, uandishi wa habari na mawasiliano, elimu ya juu, uthibitishaji wa vyeti vya halal, mafunzo ya kidiplomasia, na masuala ya kijamii na wanawake.

Mshirika mkubwa kibiashara

Uturuki na Nigeria imekuwa na uhusiano wa kidiplomasia tangu Novemba 9, 1960.

Viwango vya biashara kati ya nchi hizo mbili vimefika dola milioni 688.4 katika miezi 11 ya mwaka 2025. Pale biashara ya nishati ilipojumuishwa, Nigeria ikawa mshirika mkubwa zaidi wa Uturuki Kusini mwa Jangwa la Sahara 2025.

Makubaliano kuhusu mafunzo ya kijeshi, ulinzi, na usalama yameimarisha uhusiano wa kimkakati, huku jeshi la Anga la Nigeria likinunua ndege zisizokuwa na rubani na helikopta sita aina ya ATAK T129 kutoka Uturuki.

Makampuni ya Uturuki yamekuwa yakifanya kazi nchini Nigeria katika sekta za ujenzi, nishati, nguo, na uzalishaji, na kuuza bidhaa nje ya nchi kama za vyuma, mabati, mashine, na vyakula, wakati huo yakiagiza mafuta ghafi na bidhaa za kilimo.

Juhudi za kukabiliana na ugaidi

Zaidi ya mashirika 50 yanayomilikiwa na wafanyabiashara wa Uturuki yanafanya shughuli zake nchini Nigeria, yakiwa na jumla ya uwekezaji wa dola milioni 400.

Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya miradi iliyosimamiwa na makampuni ya ujenzi ya Uturuki imeongezeka, hadi kiwango cha karibu dola bilioni 3.

Kwa kuzingatia kwa Uturuki kuunga mkono juhudi za Nigeria za kukabiliana na ugaidi, ushirikiano katika masuala ya kijeshi, usalama, na sekta ya ulinzi kunaendelea kuimarika hatua kwa hatua.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#