Sport
Dollar
43,4040
0.09 %Euro
51,5798
0.01 %Gram Gold
7.069,9000
0.34 %Quarter Gold
11.912,4400
0 %Silver
151,1900
-0.06 %Siku ya Jumatatu Guinness World Records ilithibitisha rekodi ya mwanaharakati wa mazingira wa Kenya Truphena Muthoni ya kuvunja ile yake ya awali kwa kukumbatia mti kwa saa 72 mfululizo.
Siku ya Jumatatu Guinness World Records ilithibitisha rekodi ya mwanaharakati wa mazingira wa Kenya Truphena Muthoni ya kukumbatia mti kwa saa 72 akivunja rekodi yake mwenyewe aliyokuwa ameiweka awali.
Katika taarifa, Guinness World Records ilisema Muthoni, “mwanaharakati wa mazingira kutoka Kenya,” ametuma ujumbe mzito kuhusu kulinda mazingira yetu kwa kukumbatia mti kwa muda wa siku tatu mfululizo.
“Truphena Muthoni ameweka rekodi ya kukumbatia mti kwa muda mrefu zaidi ikiwa ni jumla ya saa 72 mfululizo,” iliongeza.
Muthoni aliweka rekodi hiyo mwezi Disemba 2025.
Rekodi ya awali ya Muthoni ilikuwa saa 48, ilhali rekodi ya kwanza ya kukumbatia mti iliwekwa 2024 na raia wa Uganda Faith Patricia Ariokot aliyekumbatia mti kwa saa 16 na sekunde 6.
Comments
No comments Yet
Comment