Dollar

43,4018

0.1 %

Euro

51,5993

0.03 %

Gram Gold

7.091,2700

0.64 %

Quarter Gold

11.912,4400

0 %

Silver

153,3800

1.39 %

Ziara ya Bola Ahmed Tinubu itaangazia ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo usalama, elimu, ustawi wa jamii, uvumbuzi, na masuala ya anga, ilisema ofisi ya rais wa Nigeria

Rais wa Nigeria Tinubu kufanya ziara Uturuki kwa mualiko wa Rais Erdogan

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu atafanya ziara rasmi nchini Uturuki kuanzia Januari 26 hadi 28 kwa mualiko wa Rais Recep Tayyip Erdogan kujadili uhusiano wa mataifa hayo mawili na kutia saini makubaliano, mkurugenzi wa mawasiliano wa Uturuki amesema Jumatatu.

Ziara ya Tinubu itajumuisha mikutano itakayoangazia kufanyia tathmini uhusiano wa Uturuki na Nigeria, kubadilishana maoni kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa, na kutia saini makubaliano yanayolenga kuimarisha ushirikiano, Mkurugenzi wa Mawasiliano Burhanettin Duran alisema katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal.

Aliongeza kuwa mkutano kati ya Rais Tinubu na viongozi wa wafanyabiashara, pamoja na majadiliano na wawakilishi wa sekta ya ulinzi, unatarajiwa kufanyika pembeni mwa ziara hiyo.

Awali, ofisi ya rais wa Nigeria ilisema ziara rasmi ya Tinubu nchini Uturuki inalenga kuimarisha uhusiano wa mataifa mawili, ikiwa na lengo la ushirikiano katika sekta ya usalama, elimu, ustawi wa jamii, uvumbuzi, na masuala ya anga.

Ziara hii inatarajiwa kujumuisha mazungumzo ya kimkakati kuhusu masuala ya fedha, mawasiliano, biashara, na uwekezaji kati ya mataifa hayo mawili.

Mikutano na maafisa waandamizi itafanyika, huku makubaliano yakitarajiwa kutiwa saini katika sekta mbalimbali ikiwemo utafiti wa kisayansi, nishati, na ushirikiano wa kijeshi.

Jukwaa la biashara litakalowaleta pamoja wawekezaji kutoka mataifa yote mawili pia litafanyika wakati wa ziara ya Tinubu.

Ziara hii inafuatia ziara rasmi ya Erdogan nchini Nigeria mwezi Oktoba 2021.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#