Dollar

43,4199

0.02 %

Euro

52,1202

-0.28 %

Gram Gold

7.308,2000

1.16 %

Quarter Gold

11.952,5300

0 %

Silver

161,2000

3.03 %

Wakazi wa kaunti ya Mandera nchini Kenya wanahofia watoto wao kufa kutokana na njaa, wakati wakichoma mifugo iliyokufa huku vyanzo vya maji vinakauka na upatikanaji wa chakula ukiendelea kuwa tatizo.

Njaa inayosababishwa na ukame kaskazini mashariki mwa Kenya yaua watoto na mifugo

Katika eneo lililokumbwa na ukame la kaskazini mashariki mwa Kenya, wanakijiji wamelazimika kuondoa mizoga ya mifugo yao kwa ajili ya kuichoma ili kuondoa harufu ya mizoga na kuwaweka mbali na makazi ya fisi.

Kaunti ya Mandera iliyo katika mpaka wa Kenya na Ethiopia na Somalia haijapata mvua tangu mwezi Mei, na hivi sasa inakaribia kuwa katika hali ya hatari ya ukame.

"Ng'ombe wangu wote na mbuzi wamekufa, na nimewachoma hapa," Bishar Maalim Mohammed, 60, mkazi wa kijiji cha Tawakal, ameiambia AFP.

Katika kijiji chake, ambapo wengi wao ni wafugaji wanategemea kwa kiasi kikubwa mifugo, ng'ombe pekee aliyebaki hawezi kusimama.

Amelala sehemu moja kwa takriban wiki nzima, akiwa hana nguvu na mifupa ikionekana, huku mmiliki wake akiangalia bila msaada wowote.

Katika mji wa karibu wa Banissa, eneo lililokuwa na uwezo wa kuwa na maji takriban lita 60,000 hivi sasa limekauka, na imekuwa sehemu ya watoto kucheza.

Mbuzi, ng'ombe na ngamia hivi sasa sharti watembezwe kwa zaidi ya kilomita 30 ili kufikia chanzo cha karibu cha maji katika kijiji cha Lulis, wakipigania maji yaliyobaki ambayo viongozi wanajaribu kuyatoa kwa mgao.

"Ndani ya wiki mbili, haya maji yatakuwa yameishi....tuko katika hali mbaya," anasema Aden Hussein, mkazi mwenye umri wa miaka 40.

Zaidi ya watu milioni mbili katika kaunti 23 za Kenya wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula baada ya mvua za mwezi Oktoba-Disemba kutonyesha.

Mamlaka ya Kitaifa ya Udhibiti wa Ukame imeziweka kaunti tisa katika tahadhari, huku Mandera ikiwa katika hatua ya 'tahadhari', hatua moja kabla ya tahadhari rasmi.

Mfumo wa mtandao wa tahadhari ya mapema hivi karibuni umesema kuwa kati ya watu milioni 20 hadi 25 nchini Kenya, Somalia na Ethiopia wanahitaji msaada wa chakula, zaidi ya nusu kwa sababu ya ukame.

"Watoto wetu ndio wanafuatia kufa," amesema Maalim Mohammed kutoka kijiji cha Tawakal.

'Hakuna maziwa kabisa'

Katika hospitali kuu ya Banissa, idadi ya watoto wenye utapiamlo imeongezeka- wengine wakifika kutoka nchi jirani ya Ethiopia — wamejaa katika wodi ya watoto.

Katika ziara ya hivi karibuni, AFP iliona watoto wanane wakiwa na tatizo la utapiamlo, ikiwemo mtoto wa miezi 32 akiwa na kilo 4.5 na mwengine aliyelazwa baada ya kurudi kutoka nyumbani bila chakula.

"Watoto hawapati lishe bora kwa sababu ya ukame...wanategemea maziwa ya ngamia na mbuzi, lakini hivi sasa hakuna maziwa kabisa," amesema Khalid Ahmed Wethow, mtaalamu wa lishe wa hospitali.

Hospitali, inahudumia takriban watu 200,000, imebaki na makopo nane tu ya maziwa ya watoto katika kitengo cha watoto, ambayo yanategemewa kuisha wiki hii.

Kitengo hicho kinategemea misaada kutoka kwa mashirika kama vile Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, lakini nchi za magharibi zinavyopunguza msaada katika kipindi cha mwaka mmoja, haijapokea chochote katika kipindi cha miezi sita.

Serikali ya Kenya na mashirika ya misaada kama vile Msalaba Mwekundu yameongeza jitihada za upatikanaji wa maji, msaada wa chakula na fedha, lakini wanasema haikidhi haja.

'Jaribio la kukimbia'

Kwa fadhaa, Bishar Mohamed, hausiani na mkazi wa kwanza, alisafiri kwa zaidi ya kilomita 150 na mifugo yake ya mbuzi 170 kutafuta malisho.

Takriban 100 ilikufa njiani na wengine walikufa baada ya kurudi nyumbani katika kijiji cha Hawara.

"Tumejaribu kuondoka kutafuta sehemu nzuri lakini tumeshindwa," ameiambia AFP, akisimama katika eneo ambalo mizoga ya mifugo yake imekusanywa.

"Nimekuwa nikitembea kwa miguu...kichwa kinaniuma...tuna kiu."

Katika kijiji cha karibu cha Jabi Bar, uandikishaji wa watoto shule umeshuka takriban kwa nusu, mkuu wa shule Ali Haji Shabure ameiambia AFP.

"Watoto 99 pekee ndio waliopo shule, wengi wameondoka na wazazi wao," amesema Shabure.

Mvua nyengine, iwapo zitanyesha, ni kabla mwezi Aprili.

Bishara Maalim, mama wa watoto 10 katika kijiji cha Hawara, ana tumaini moja tu kwa watoto wake: "Mungu waokoe."

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#