Dollar

43,4313

0.02 %

Euro

52,1184

-0.29 %

Gram Gold

7.312,7400

1.22 %

Quarter Gold

11.952,5300

0 %

Silver

161,1300

2.98 %

Rais aliyechaguliwa nchini Guinea Mamady Doumbouya amemteua waziri mkuu kwa serikali ya taifa hilo ya Afrika Magharibi ikiwa chini ya wiki mbili tangu alipoapishwa rasmi.

Rais wa Guinea Doumbouya amthibitisha waziri mkuu mpya

Rais wa Guinea aliyechaguliwa Mamady Doumbouya amemteua waziri mkuu kwa serikali ya taifa hilo la Afrika Magharibi chini ya wiki mbili baada ya kuapishwa.

Amadou Oury Bah, ambaye amewahi kuwa waziri mkuu kuanzia Februari 2024 hadi Januari 2026 wakati wa kipindi cha mpito, ataendelea kuwa katika nafasi hiyo chini ya serikali mpya, kulingana na agizo lililosomwa katika televisheni ya taifa Jumatatu jioni.

Doumbouya alichaguliwa mwishoni mwa mwezi Disemba na kuapishwa rasmi kuwa rais Januari 18 kwa muhula wa miaka saba, ambao unafuata miaka minne aliyokuwepo madarakani baada ya mapinduzi dhidi ya Rais Alpha Conde 2021.

katika agizo hilo, Doumbouya pia alitangaza kuwa serikali yake itajumuisha wizara 27 na makatibu wakuu wawili. Uteuzi wao unatarajiwa kufanyika katika siku zijazo.

Katiba mpya

Mwishoni mwa mwezi Septemba 2025, raia wa Guinea waliidhinisha katiba mpya katika kura ya maoni, kutoa fursa kwa Doumbouya kushiriki katika uchaguzi.

Pia iliongeza mihula ya urais kutoka miaka mitano hadi saba, kwa mihula miwili tu.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#