Dollar

43,4293

0.02 %

Euro

52,1720

-0.2 %

Gram Gold

7.315,3500

1.26 %

Quarter Gold

11.952,5300

0 %

Silver

160,7700

2.75 %

Shambulizi hilo katika kituo muhimu cha wahamiaji ni dhihirisho la shinikizo kwa mataifa ya Sahel wakati wakianzisha kikosi kipya cha kanda.

Mashambulizi ya silaha yawaua watu 10 katika kituo cha polisi cha Niger karibu na mpaka wa Algeria

Maafisa wa usalama wa Niger wasiopungua 10 wameuawa wakati watu wenye silaha walipovamia kituo cha polisi kaskazini mwa Niger, eneo lliilokumbwa na vurugu na ulanguzi wa watu katika mpaka, vyombo vya habari vya Ufaransa vilisema siku ya Jumanne.

Mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya polisi huko Assamaka, mji wa jangwa katika na mpaka wa Algeria ambao huwa ni njia kuu kwa wahamiaji wa Afrika Magharibi wanaoelekea kaskazini, kulingana na Radio France Internationale (RFI).

Watu wenye silaha walikuwa kwenye magari sita na kushambulia kituo cha polisi siku ya Jumatatu, vyanzo vya usalama vya Niger viliviambia chombo hicho cha habari. Washambuliaji wawili waliuawa katika makabiliano hayo, vyanzi hivyo vilisema.

Hakuna kundi lililokiri kuhusika na tukio hilo.

Vikosi vya pamoja dhidi ya makundi ya kigaidi

Vurugu hizo zinatokea wakati Niger, Mali na Burkina Faso zikijitahidi kuimarisha ushirikiano wa kiusalama chini ya mpango wa vikosi vya pamoja unaolenga kukabiliana na makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel.

Disemba 20, nchi hizo tatu zilianzisha rasmi Muungano wa Mataifa ya Sahel (FU-AES), kikosi cha maafisa 5,000 ambacho kitafanya operesheni ya pamoja dhidi ya ugaidi, kuimarisha usalama mpakani na kuongeza kupeana taarifa za kiintelijensia.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#