Dollar

38,7901

0.03 %

Euro

43,3966

0.8 %

Gram Gold

4.058,6700

0.58 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kwa miezi kadhaa, kampeni ya Tidjane Thiam ya kuwania urais imekumbwa na wasiwasi kuhusu uraia wake.

Kiongozi wa upinzani Côte d'Ivoire Thiam ajiuzulu kufuatia utata wa uraia wa Ufaransa

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Côte d'Ivoire, ambaye amezuiliwa kugombea urais katika uchaguzi wa Oktoba, amesema Jumatatu kuwa anajiuzulu kama kiongozi wa upinzani lakini bado ataongoza kampeni ya kushinda uchaguzi.

Ni miezi sita kabla ya uchaguzi wa kumchagua kiongozi mpya wa nchi, kuna taharuki ya kisiasa katika nchi hiyo ya Afrika magharibi ambapo wagombea wengi wa upinzani wameondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi.

Kwa miezi kadhaa, kampeni ya Tidjane Thiam ya kuwania urais imekumbwa na wasiwasi kuhusu uraia wake.

Mahakama moja mjini Abidjan iliondoa jina lake kwenye daftari la wapiga kura mwezi uliopita, ikisema mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 62 alipoteza uraia wake wa Cote d’Ivoire alipochukua uraia wa Ufaransa 1987.

Thiam, ambaye hajakuwa nchini Côte d'Ivoire kwa zaidi ya mwezi mmoja, pia anakabiliwa na kesi dhidi ya kuchaguliwa kwake kama kiongozi wa chama cha Democratic Party of Côte d'Ivoire (PDCI).

Kesi iliwasilishwa na mwanachama ambaye pia anatilia shaka uraia wa Thiam wakati alipochaguliwa kuwa mgombea wa urais.

Sakata la uraia pacha

"Kwa maslahi ya chama, nimeamua kuwaachia nyinyi majukumu yangu ya rais wa chama, wanaharakati," Thiam alisema katika hotuba yake iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii.

Lakini mfanyakazi huyo wa zamani wa benki, ambaye bado ni makamu wa rais wa chama, ameweka wazi kuwa uamuzi wake wa kung’atuka siyo eti ni kujiondoa katika mapambano ya kuwania urais.

"Uamuzi huu haubadilishi dhamira niliyoitangaza Disemba 2023 kwa mimi mwenyewe kuongoza chama chetu kupata ushindi Oktoba 2025," alisema.

"Najuwa baada ya kunichagua mimi 2023, mtaniamini na jukumu hilo tena," aliongeza.

Wagombea wa urais hawaruhusiwi kuwa na uraia pacha. Thiam alizaliwa Côte d'Ivoire na kujivua uraia wa Ufaransa mwezi Machi ili aweze kugombea urais.

Kumuondoa kwenye orodha ya wapigaji kura, hukumu ya mahakama iliegemea kifungu cha 48 kuhusu kanuni ya uraia, ambayo imekuwepo tangu katika miaka ya 1960.

Kiongozi mpya wa chama

Kanuni inasema kuwa ukiwa raia wa taifa lingine kunamaanisha kujivua uraia wa Cote d’Ivoire.

Kufuatia tangazo la Thiam, makamu wa rais wa chama cha PDCI Ernest N'Koumo Mobio anakaimu uongozi wa chama hicho.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 92 ametoa wito wa kuwepo "mshikamano, utulivu na nidhamu" na kutaka kuwepo kwa mkutano wa chana mapema Jumatatu ili "kujadili masuala muhimu kuhusu hali ya kisiasa".

Afisa mwandamizi wa chama cha PDCI anasema mkutano huo utatoa fursa ‘‘kwa chama kusisitiza kumuunga mkono" Thiam.

Karibu wanachama 100 walikusanyika siku ya Jumatatu katika makao makuu ya chama ambapo pia kulikuwa na maaskari wa kukabiliana na ghasia. Wanachama hao walikuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa : "Usiingilie haki yangu ya kupiga kura", Mwandishi wa habari wa AFP aliyaona.

Viongozi wengine watatu wa upinzani pia wameondolewa kwenye kugombea urais, ikiwemo rais wa zamani Laurent Gbagbo kutokana na kupatikana na hatia na mahakama.

"Tulikuwa na matumaini ya kuwepo kwa uchaguzi utakaojumuisha kila mtu, wa uwazi na wa amani, ni wazi kuwa kuondolewa kusiko na haki kwa mgombea wa PDCI ni sehemu ya njama ya kuwaondoa wagombea wakuu wa upinzani ili kuhakikisha wanapanga uchaguzi na kupata ushindi wa mchongo," Thiam alisema Jumatatu.

Mara nyingi mamlaka hukanusha madai yoyote ya kuingiliwa kisiasa katika mchakato wa uchaguzi, zikisema maamuzi yanafanywa na mahakama iliyo huru.

Rais Alassane Ouattara, 83, ambaye amekuwepo madarakani tangu 2011, bado hajasema kama atagombea tena urais lakini anasema ana hamu ya "kuendelea kutumikia nchi yangu".

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#