Dollar

38,7761

-0.01 %

Euro

43,2227

0.43 %

Gram Gold

4.031,7600

-0.09 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Wazalsihaji wanadai kuwa uuzaji wa nafaka kwa nchi nyengine zimesababisha viwanda kufungwa na madalali kupata faida badala ya wakulima.

Wazalishaji Uganda wataka nafaka isiuzwe nje ya nchi

Chama cha wazalishaji nchini Uganda kimeitaka serikali kupiga marufuku uuzaji wa nafaka mbichi nje ya nchi kwa nia ya kuwalinda wakulima wa ndani.

Wanadai hii ni kwa nia ya kuwalinda dhidi ya unyanyasaji na kukuza ukuaji wa viwanda vya ndani.

“Wafanyabiashara wa Kenya wananunua mahindi moja kwa moja kutoka mashambani wakiyavuna wenyewe na kuyasafirisha wenyewe kuvuka mipaka. Wakulima hawafaidiki na bei ya juu, ni madalali tu ndio wanafaidika,” Alziema John jet Tusabe, mwakilishi wa chama cha wazalishaji.

Wazalishaji hao walikuwa katika Kamati ya Bunge ya Uganda ya Fedha iliyokuwa inaangalia mswada unaohusu mauzo ya nje.

Muswada huo unapendekeza kuwe na kodi ya dola 10 kwa kila tani kwa mauzo yanayotokana na ngano, pamba na mahindi.

Wazalishaji wa viwanda wanadai kodi hiyo haitamsaidia mkulima wa ndani.

“Uganda haikosi tu fedha ila pia inaathiri viwanda vya ndani vinavyohitaji bidhaa hizi. Nchi nyengine zinatetea mali ghafi yake, Uganda lazima ifanye hivyo pia,” Tusabe aliongezea.

Chama cha wenye viwanda kimetoa mfano wa kiwanda cha Mukwano kilichopo Lira, kaskazini mwa nchi kilichofungwa kwa sababu ya kukosa mbegu ya mafuta, mbegu za alizeti na soya, muhimu kwa ajili ya kuzalisha mafuta ya kupikia.

“Zaidi ya kuzalisha mafuta ya mboga pia tunazalisha bidhaa ya protini inayotumika katika chakula cha mifugo,” Alielezea Tony Gadhore, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni za Mukwano.

“Sasa inatulazimu kununua soya kutoka nje ya nchi ili kudumisha uzalishaji. Sio kampuni yetu ya Mukwano tu, viwanda vingi vinalazimika kununua nafaka kutoka nchi za nje, kwa sababu tunapoteza nafaka zetu kwa nchi jirani,” Gadhore alisema.

Mjadala huo unafanyika huku ripoti ya hivi majuzi ya wizara ya fedha zikionyesha Uganda ilivutia mapato ya dola milioni 843.85 kwa mauzo yake ya nje, mwezi Februari 2025, ikilinganishwa na dola milioni 887 iliyolipa kwa kuagiza bidhaa kutoka nchi zingine.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#