Dollar

38,7715

-0.02 %

Euro

43,2687

0.53 %

Gram Gold

4.038,9200

0.09 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Tangazo hilo linakuja mwezi mmoja baada ya serikali kuweka tarehe 21 Septemba 2025 kuwa siku ya kura ya maoni ya katiba, ambayo ilisema itakuwa utangulizi wa kurejea kwa utawala wa kikatiba.

Serikali ya kijeshi ya Guinea yatangaza tarehe mpya ya uchaguzi

Waziri Mkuu wa Guinea, nchi inayoongozwa na jeshi, ametangaza tarehe mpya ya Disemba 2025 kwa ajili ya uchaguzi, akitaka kuwatuliza wawekezaji katika hotuba yake kwenye kongamano la wafanyabiashara barani Afrika siku ya Jumatatu.

Guinea Conakry inatawaliwa na kiongozi wa kijeshi Mamady Doumbouya, ambaye alichukua mamlaka katika mapinduzi ya Septemba 2021, na mwaka 2022 alipendekeza serikali ya mpito wa miaka miwili kuelekea uchaguzi lakini hakuandaa kura.

Baadaye wanajeshi waliweka lengo la Disemba 31, 2024 la kurudisha utawala wa kiraia, lakini lengo hilo halikutekelezeka.

Waziri Mkuu Amadou Oury Bah alitangaza tarehe hiyo mpya siku ya Jumatatu katika Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji wa Afrika mjini Abidjan, Ivory Coast, wakati akizungumza kuhusu mradi wa chuma wa Simandou wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kura ya maoni kwanza

Tangazo hilo linakuja mwezi mmoja baada ya serikali kuweka tarehe 21 Septemba 2025 kuwa siku ya kura ya maoni ya katiba, ambayo mamlaka imesema itakuwa utangulizi wa uchaguzi na kurudi kwa kanuni ya kikatiba.

"Kura ya maoni ya katiba itakuwa Septemba 21 na uchaguzi wa wabunge na urais utakuwa Disemba," alisema Waziri Mkuu.

Mnamo Julai 2024 junta iliwasilisha rasimu ya katiba mpya ambayo inaweza kumruhusu Doumbouya kushiriki katika uchaguzi ujao wa urais.

Vyama viwili tawala vya zamani vya Guinea vimesimamishwa kwa sasa.

Chama chengine kikuu cha upinzani, Union of Democratic Forces of Guinea, kimewekwa chini ya uangalizi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#