Sport
Dollar
38,7752
0 %Euro
43,3731
0.77 %Gram Gold
4.047,9000
0.31 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Ujasusi nchini Kenya amesema vikosi vya usalama vimekuwa na changamoto ya kifedha kwa muda mrefu na haviwezi kupata vifaa vya kisasa vya ulinzi.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Ujasusi nchini Kenya, Noordin Haji amelitaka Bunge kuhakikisha kuwa kuna fedha za kutosha kwa vyombo vya usalama vya Kenya, akionya kwamba juhudi za ulinzi wa kitaifa zinaweza kudhoofika ikiwa upungufu wa bajeti utaendelea.
“Tunakumbwa na hatari kutoka kwa majirani wetu, labda isipokuwa kutoka Tanzania,” Haji aliiambia Kamati ya Idara ya Ulinzi, Upelelezi na Mahusiano ya Nje.
“Ukiangalia Uganda kuna Karamajong' na makabila mengine yanayoingia Kenya kufanya wizi wa ng'ombe. Wamevamia baadhi ya ardhi zetu. Sudan Kusini kuna kuenea kwa silaha ndogo ndogo, hatuna budi kukabiliana na hilo," aliongezea.
Amesema vikosi vya usalama vimekuwa na changamoto ya fedha kwa muda mrefu na haviwezi kupata vifaa vya kisasa vya ulinzi.
"Nchini Ethiopia kuna Jeshi la Ukombozi la Oromo, OLF, wanakalia eneo letu na tunalazimika kushughulika nao lakini ukiangalia aina ya vifaa ambavyo tunavyo kama sekta ya usalama ni kweli havitoshi, na nadhani kama nchi tunapaswa kuamua ikiwa tuko makini na kama tunataka kuhakikisha kuwa tunatoa usalama unaostahili Kenya."
Haji alidai zaidi kwamba jeshi, kwa mfano, halijapokea vifaa vyao vinavyohitajika kwa miaka 10 iliyopita.

Aliieleza kamati hiyo kuwa makadirio ya bajeti ya sekta hiyo yanahitaji kupewa kipaumbele ili kumaliza mgogoro huo.
Awali NIS ilikuwa imeomba zaidi ya dola milioni 500 ( Ksh.65 bilioni), lakini bajeti ilipunguzwa hadi zaidi ya dola milioni 395 ( Ksh.51 bilioni).
Hapo awali, Waziri wa Ulinzi Patrick Mariru aliiambia kamati hiyo kwamba ufadhili mdogo pia umeinyima wizara fursa ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
"KDF( Jeshi la Taifa) imeshindwa kuajiri kwa miaka miwili iliyopita ya fedha. Hii si nzuri kwa kikosi hicho, kwa hivyo mwaka huu KDF lazima ifanye kazi ya kuajiri na tunaitaka kamati hii itusaidie kupata rasilimali zinazohitajika kufanya hivyo," alisema Katibu Mkuu Mariru.
Alifafanua pia kuwa KDF inahitaji takriban dola milioni 15. 4 (Ksh. 2 bilioni) ili kuajiri mwaka huu, na kuongeza kuwa afisa aliyeajiriwa anahitaji takriban dola 15,000 (Ksh.2 milioni) kwa mafunzo ya miezi 9.
Comments
No comments Yet
Comment