Sport
Dollar
38,5992
0.33 %Euro
43,6545
0.2 %Gram Gold
4.017,2800
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Msemaji wa jeshi la Sudan amesema vikosi vya RSF vimelenga kambi ya jeshi la anga na miundombinu mengine karibu na eneo la uwanja wa ndege uliopo Port Sudan
Msemaji wa Jeshi la Sudan amesema vikosi vya wapiganaji vya RSF vimelenga kwa mashambulizi kambi ya jeshi la anga pamoja na miundombinu mengine iliyopo karibu na eneo la uwanja wa ndege wa Port Sudan.
Haya yanajiri wakati Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu ya Sudan siku imetangaza kuuawa kwa raia wasiopungua 300, ikiwemo watoto 21 na wanawake 15, katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi la RSF katika mji wa Al-Nahud kwenye jimbo la Kordofan Magharibi.
Katika taarifa rasmi, tume hiyo imelaani tukio hilo na kusema ni “ukiukwaji mkubwa uliotekelezwa na kundi la RSF dhidi ya raia wa Al-Nahud, ikiwemo kuwalenga kwa makusudi, kuwapiga risasi kwa karibu, na kuwaua.”
Tume pia ilisema kuwa idadi hiyo ya vifo ni ya muda tu kwa sasa kwa sababu bado mashambulizi yanaendelea katika mji huo kwa sababu wapiganaji wa RSF wanazuia misaada kuingia na kutoruhusu watu kuondoka eneo hilo.
Comments
No comments Yet
Comment